The House of Favourite Newspapers

Takukuru yakamilisha ushahidi kesi ya Matandika, Chacha

juma-matandika-2

Juma Matandika

Omary Mdose | CHAMPIONI, Dar es Salaam

ILE kesi inayowakabili waliokuwa maofisa wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Martin Chacha na Juma Matandika ya kutuhumiwa kuomba rushwa ya Sh milioni 25, jana Ijumaa upande wa mashtaka ulikamilisha ushahidi wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Shahidi wa mwisho ambaye ni Johnson Gibson Kisaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Kitengo cha Uchunguzi wa Kimaabara wa Elektroniki, jana alitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu, Huruma Shaidi.

Shahidi huyo ndiye aliyehusika kuhamisha sauti zinazodaiwa kuwa ni za watuhumiwa kutoka kwenye simu ya mmoja wa mashahidi, Salum Kurunge na kuiweka katika CD iliyowasilishwa mahakamani hapo kama kielelezo.

Kutokana na kukamilika kwa ushahidi wa pande zote mbili, hukumu ya kesi hiyo inatarajiwa kutolewa Februari 24, mwaka huu.

Ikumbukwe kuwa, Chacha na Matandika wanakabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya Sh milioni 25 kutoka kwa viongozi wa timu ya Geita Gold Sports iliyokuwa ikishiriki Ligi Daraja la Kwanza msimu uliopita, Constantine Moland na Salum Kurunge.

Matandika na Chacha wanatuhumiwa kuomba rushwa hiyo kwa viongozi hao wa Geita ambao ni Constantine Molandi na Kurunge ili wawasaidie kusikilizwa kwa rufaa yao waliyoipeleka TFF Februari 5, mwaka jana.

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.