The House of Favourite Newspapers

Taliban Waua Watu 13 Afghanistan

0

Takribani wanajeshi 13 wa Afghanistan wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa wakati wapiganaji wa Taliban walipovishambulia vituo vya ukaguzi wa usalama katika mkoa wa kaskazini wa Kunduz.

 

Maafisa wamesema wanajeshi wanane na karibu polisi wanne wamejeruhiwa katika shambulizi hilo huku wengine wakichukuliwa mateka na wanamgambo hao wa Taliban. Shambulizi hilo lilifanywa katika wilaya ya Dasht-e Archi.

 

Mkuu wa Wilaya hiyo Saddudin Sayyed amesema kuwa hadi sasa vituo hivyo vya ukaguzi vimerejeshwa katika udhibiti wa vikosi vya serikali.

 

Leave A Reply