The House of Favourite Newspapers

Tambwe Aonyeshwa Mlango wa Kutokea Yanga

0

Sweetbert Lukonge | CHAMPIONI| Dar es Salaam

STRAIKA wa Yanga, Amissi Tambwe, huenda msimu ujao asionekane katika kiko­si cha timu hiyo kutokana na kutojua hatima yake ndani ya klabu hiyo mpaka sasa.

Tambwe ambaye ameon­goza Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara tatu mfululizo tangu alipojiunga nayo msimu wa 2014/15 akitokea Simba, ame­liambia Championi Ijumaa kuwa kwa jinsi mambo yanavyoenda inawezekana asiitumike timu hiyo msimu ujao.

Alidai kuwa mpaka sasa hakuna chochote kina­choendelea kati yake na uongozi, hivyo kama hali hiyo itaendelea mpaka mwezi Julai, basi ata­chukua uamuzi wa kwen­da kutafuta maisha sehe­mu nyingine katika timu ambazo zimeonyesha nia ya kutaka kusajili za hapa nchini na nje ya nchi.

Kwa sasa Tambwe amei­fungia Yanga mabao 46 katika michuano ya ligi kuu tangu alipojiunga nayo, yupo kwao nchini Burundi kwa ajili ya mapumziko na hajui lini atarejea nchini.

“Kwa hiyo, kutokana na hali hiyo sijui nitarejea lini nchini, lakini ninachoweza kusema ni kwamba bado ninaipenda Yanga na ndiyo maana nimeamua kusitisha mipango yangu mingine mpaka niwasikilize wao kwanza.

“Lakini wakiendelea kuwa kimya mpaka Julai basi ni­tachukua uamuzi mwingine kwa sababu soka ndiyo kazi yangu, naweza kujiunga na timu yoyote hapo nchini au nje ya nchi ambazo tangu zamani zimekuwa zikinihi­taji,” alisema Tambwe am­baye mkataba wake na Yan­ga tayari umeshamalizika.

 

==============================

GLOBAL TV Online, Kupitia kipindi chake cha Michezo, SPOTI HAUSI, imezungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Timu ya Soka ya Simba Sport Club, Zacharia Hans Poppe ambaye amefunguka mengi kuangazia klabu yake na soka la bongo kwa ujumla.

FUATILIA MAHOJIANO HAYO HAPA

Leave A Reply