The House of Favourite Newspapers

Tambwe atua Dar kimyakimya kumalizana na Yanga SC

0

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe, amewasili nchini Ijumaa iliyopita kumalizana na viongozi wake hao kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu.

Tambwe ni miongoni mwa wachezaji kadhaa wa Yanga waliomaliza mikataba, akiwemo

Deogratius Munishi ‘Dida’, Deus Kaseke, Vincent Bossou, Donald Ngoma, Anthony Matheo, Thabani Kamusoko na Malimi Busungu.

 

Wengine ni pamoja na Haruna Niyonzima anayetarajiwa kusaini Simba na Oscar Joshua lakini Mwinyi Haji tayari ameshajifunga mkataba wa miaka miwili ya kuitumikia timu hiyo.

 

Taarifa ambazo Championi Jumatatu limezipata kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa, mshambuliaji huyo tayari yupo nchini anaendelea na mazungumzo ya kuongeza mkataba mwingine ambapo kila kitu kinakwenda sawa.

 

“Tambwe ametua nchini tangu Ijumaa ambapo yupo hapa anafanya mazungumzo na uongozi kwa ajili ya kuongeza mkataba mwingine wa kuitumikia Yanga.

“Mazungumzo yanaendelea vizuri na iwapo tutakubaliana, basi atamwaga wino,” kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa Tambwe, alikiri kuwa yupo nchini tangu juzi jioni.

 

“Kweli nimefika nchini lakini nilikuwa nimezima simu kwa kuwa watu walikuwa wananisumbua,” alisema Tambwe na alipoulizwa hatima yake ya kuongeza mkataba Yanga, alisema atafutwe baadaye. Gazeti hili bado linaendelea kuchimba kuhusiana na suala hilo.

 

Khadija Mngwai na Sweetbert Lukonge | CHAMPIONI | Dar

Leave A Reply