The House of Favourite Newspapers

Tambwe awapagawisha Yanga

ALICHOKIFANYA, Amissi Tambwe juzi Jumatatu huko jijini Mbeya alipoiongoza Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Prisons kimezua balaa makao makuu ya klabu hiyo. Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa Tambwe alionyesha kiwango cha hali ya juu pamoja na kwamba hakucheza kwa dakika 90. Katika mabao yote matatu ya Yanga Tambwe alihusika.

 

Tambwe alifunga mawili, lakini lile la penalti ambalo lilifungwa na Ibrahim Ajibu yeye ndiye aliangushwa kwenye boksi. Kutokana na hali hiyo, Nahodha Msaidizi wa Yanga, Juma Abdul ameliambia Championi Jumatano kuwa, sasa Tambwe ameanza kurudi katika kiwango chake ambacho kila mtu anakijua.

 

“Kama uliona hata baada ya mechi kumalizika kila mchezaji, viongozi, mashabiki wote kwa pamoja walimfuata Tambwe kumpongeza japokuwa aliingia uwanjani akitokea benchi lakini alifanya kazi kubwa, hakika tunampongeza kwa hilo lakini pia tuendelee kupambana kwa ajili ya timu yetu,” alisema Abdul ambaye staili yake ya uchezaji haimvutii Mwinyi Zahera licha ya kuwa alikuwa majeruhi.

 

Zahera alisema kuwa: “Nampongeza Tambwe kwa kazi nzuri aliyoifanya katika mechi hiyo, kwani maagizo niliyompa akayafanye baada ya kumtoa Juma Abdul aliyafanya kwa asilimia zaidi ya 90, nimwombe tu aendelee kujituma mazoezi ili aweze kuwa fiti zaidi ya alivyo sasa.”

Sweetbert Lukonge

Comments are closed.