The House of Favourite Newspapers

Tambwe: Pluijm ananizuia kufunga

0

tambweSaid Amissi Tambwe

Ally, Dar es Salaam

LICHA ya kufunga mabao 21 katika Ligi Kuu Bara msimu huu, straika wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe ametamka kuwa sababu kubwa inayomfanya kushindwa kung’ara katika michuano ya kimataifa ni kutokana na kocha wake, Hans van Der Pluijm kumuhamisha nafasi.

Tambwe ambaye tangu timu hiyo ilipokuwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika mpaka sasa Kombe la Shirikisho Afrika, amefunga bao moja tu dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius tofauti na straika mwenzake, Donald Ngoma ambaye ana mabao matatu.

Akizungumza na Championi Jumatano, Tambwe alisema kuwa katika michuano ya kimataifa, Pluijm amekuwa akimuhamisha nafasi na kumchezesha nyuma ya mshambuliaji (Ngoma) ambapo kiasili yeye hajazoea kuicheza nafasi hiyo.

“Siyo kama sina makali katika michuano ya kimataifa, bali ukweli ni kwamba nimekuwa nikibadilishwa namba (nafasi) na majukumu ambapo kocha ananitumia kama mshambuliaji wa pili na mbele yangu anakaa Ngoma (Donald).

“Sasa mimi siwezi kuicheza namba ile kikamilifu ambayo inanilazimu kuzunguka karibu nusu ya uwanja, sasa mpaka nafika katika goli la wapinzani nakuwa nimeshachoka ndiyo maana hata ninapokuja kufanya shambulizi linakuwa linakosa nguvu.

“Lakini nitaendelea kupambana katika michezo ijayo kuhakikisha nafunga na kuniweka katika mazingira ya kujitangaza zaidi Afrika na duniani kwani kama unavyojua mashindano hayo yanafuatiliwa na watu wengi wa soka,” alisema Tambwe.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: globaltvonline

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply