The House of Favourite Newspapers

Tambwe ampa Kagere mbinu awe mfungaji bora Caf

Meddie Kagere

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe ametoa darasa la kutosha kwa mshambuliaji wa Simba, Mnyarwanda, Meddie Kagere kama anataka kuwa mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

 

Tambwe ametoa darasa hilo kutokana na Moataz Al-Mehdi wa Al-Nasr ya Libya anayeongoza kwa kufunga mabao saba timu yake imeshatoka akifuatiwa na Kagere mwenye mabao matano huku Mzambia, Clatous Chama na Jean Marc Makusu Mundele wa As Vita ya DR Congo AS Vita wakiwa na mabao manne.

Amissi Tambwe

Mshambuliaji huyo aliyewahi kucheza Simba akitokea Vital O ya Burundi, alisema kuwa, Kagere kwa sasa anaweza kuwa mfungaji bora wa Afrika iwapo atajiwekea malengo ya kufunga katika kila mechi ya hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa kuwa bado wana nafasi kubwa ya kucheza robo fainali.

“Kagere naona anaweza kuwa mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa lakini kama ataendelea kufunga katika kila mechi ila kama atakuwa amejiwekea malengo ya kufanya hivyo kwa sababu inawezekana.

 

“Unajua ukiangalia hapa tayari mtu anayeongoza kwa kufunga ameshatoka, sasa hapa Kagere anatakiwa kufunga kwanza kwenye mechi inayokuja ikiwezekana hata bao moja apate ili apunguze idadi halafu kwenye mechi za hapa aifanye kazi yake vizuri,” alisema Tambwe.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.