The House of Favourite Newspapers

Tamu ya Mastaa Mwaka 2019

0

WAKATI tukisubiri kwa shauku kubwa kuingia Mwaka Mpya wa 2020, si vibaya tukajiku-mbusha machungu na matamu waliyopitia mastaa wetu kwa mwaka 2019.

Wapo waliopitia raha na furaha, lakini wapo waliopitia kwenye karaha na misukosuko hasa kwenye eneo la uhusiano wa kimapenzi;

 

STEVE NA WELLU

Huyu ni mwigizaji wa filamu na vichekesho Bongo ambaye alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji mwenzake ‘tipwa’, Wellu Sengo ‘Matilda’ ambaye kwa sasa anatamba kwenye Tamthiliya ya Rebeca.

Kabla ya kukarah-ishana na kuten-gana mwaka 2019, wawili hawa walija-aliwa mtoto mmoja wa kike. Hawa walionja chungu ya mwaka 2019 baada ya kutengana na sasa kila mmoja ana maisha yake.

 

JUX NA VANESSA

Hawa ni wanamuziki wa Bongo Fleva ambao walidumu kwa miaka mingi kwenye uhusiano wa kimapenzi kama wachumba sugu.

Kuna kipindi walia-chana kisha wakaru-diana, wakaa-chana tena kisha wakaru-diana, lakini mwaka 2019 walionja joto la jiwe baada ya kuachana jumla.

 

Baada ya hapo, Jux aliangukia kwenye penzi la mrembo kutoka nchini Thailand ambaye kuna za chinichini kwamba, naye ameachana naye.

Kwa upande wake Vanessa, moyo wake ulitua kwa mwigizaji wa Marekani, Rotimi ambaye wametangaza kufunga ndoa ya kihistoria.

 

KIBA NA AMINA

Mkali huyu wa Bongo Fleva, mwaka 2019 alikutana na kasheshe ya aina yake baada ya ndoa yake na Amina Khaleef wa Mombasa nchini Kenya kudaiwa kuvunjika. Hayo yalijiri miezi michache baada ya wawili hao kujaaliwa mtoto wa kiume, Keyaan. Kwa mujibu wa Kiba, hadi sasa Amina yupo kwao.

 

MONDI NA TANA-SHA

Kinara huyu wa Bongo Fleva, yeye alijikuta akionja tamu ya penzi jipya na mtangazaji wa Kenya, Tanasha. Wawili hawa walijaaliwa mtoto wa kiume, Naseeb Junior.

 

BEN POL NA ANERLISA

Mkali huyu wa miondoko ya RnB Bongo aliokota dodo baada ya kuanza kufaidi utamu wa penzi la mrembo bilionea wa nchini Kenya, Arnelisa Muigai.

Wawili hawa walidai kufunga ndoa ya kimila na sasa wanasubiri kufunga ndoa ya kihistoria.

 

MBOSSO NA RUKIA

Jamaa huyu alikutana na uchungu na utamu ndani ya mwaka 2019. Ukiacha machungu ya kufiwa na aliyekuwa mpenzi na mzazi mwenzake, mchekeshaji Boss Martha, lakini pia alijaaliwa kupata mtoto wa kiume na mdada wa mjini, Rukia Rucky waliye-mpa jina la Iqram Khan.

 

RAY-VANNY NA FAHYMA

Mkali huyu mwingine kutoka Lebo ya WCB alijikuta akionja chungu baada ya kutengana na mwandani wake, Fahyma ambaye ni mama wa mtoto wake wa kiume aitwaye Jaydan.

Ilisemekana kuwa, chanzo cha wawili hawa kutengana ni kitendo cha Rayvanny kudaiwa kuchepuka na video vixen aliyemtumia kwenye video yake ya I Love You aitwaye Nana.

 

MLELA NA EBITOKE

Mahaba yao yalikuwa ni moto wa kuotea mbali kabla ya kukutana na machungu.

Uhusiano wao uliingia shubiri baada ya Ebitoke kumvamia Mlela hotelini alipokuwa na mkutano na waandishi wa habari kisha kumfanyia fujo akidai kumsaliti na mrembo aliyetajwa kwa jina la Stella au Beyonce.

Baada ya hapo, Mlela aliendelea na Stella huku Ebitoke naye akitamba na kidume mpya aitwaye Simko.

 

PETIT MAN NA ESMA

Hawa walionja machungu baada ya ndoa yao kuvunjika huku wakiwa wame-jaaliwa mtoto mmoja wa kike aitwaye Taraj ambapo kila mmoja alijikuta kwenye penzi na mtu mwingine.

Hata hivyo, baadaye walirudiana na maisha yao yanaendelea sawia.

 

JIDE NA GARDNER

Hawa walijikuta wakifurahia maisha baada ya kusemekana wame-rudiana baada ya ndoa yao kuvunjika muda mrefu.

 

AUNT NA IYOBO

Mwanamama huyu mwigizaji alijikuta akionja machungu baada ya kutengana na baba mtoto wake huyo. Baadaye walirudiana na kuendelea kumlea mtoto wao, Cookie.

 

NIKKI NA JOAN

Mkali huyu wa Hip Hop Bongo, mwaka 2019 alivunja ukimya baada ya kumchumbia mpenzi wake wa kitambo aitwaye Joan. Pia walionja utamu wa penzi lao baada ya kujaaliwa mtoto wa kike waliyempa jina la Zuri.

 

G-NAKO NA YASINTA

Mwaka 2019 ulikwenda poa kwa mkali huyu wa korasa baada ya kumchumbia mwandani wake huyo wa kitambo ambaye wamejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kike aitwaye Gianna. G-Nako au Warawara alitarajia kufunga ndoa na Yasinta wikiendi iliyopita. 

Leave A Reply