The House of Favourite Newspapers

Tanesco Watoa Tamko Kuhusu Hitilafu Iliyojitokeza Katika Gridi ya Taifa

0


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linautaarifu umma kuhusu hitilafu iliyojitokeza katika Gridi Taifa leo tarehe 08 Disemba 2023 majira ya saa 04:14 asubuhi, hitilafu hiyo ilipekea mikoa inayopata umeme kutoka katika Gridi ya Taifa kukosa umeme.

Hitilafu imetokana na kusombwa na maji nguzo kubwa za kusafirisha umeme kutoka katika Kituo cha kuzalisha umeme kwa gesi asilia cha Ubungo III eneo la Mto Gide, Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. Uharibifu huo umepelekea kutoka kwa Gridi ya
Taifa.
Umeme kwa sasa umeanza kurejea kwa awamu katika mikoa iliyokuwa inakosa umeme na jitihada zinaendelea kuhakikisha mikoa yote inapata umeme mapema iwezekanavyo.
Aidha, jitihadi nyingine zinazofanywa na Shirika ni kuhakikisha miundombinu iliyoharibika inajengwa ndani ya muda mfupi, kuruhusu kusafirisha umeme unaokosekana katika Gridi ya Taifa kutoka Kituo cha kuzalisha umeme kwa gesi asilia
cha Ubungo III.
Shirika linawaomba radhi kwa kwa usumbufu uliojitokeza, na litaendelea kutoa taarifa za hali ya upatikanaji wa umeme kwa kadri hali itavyozidi kuimarika.
Imetolewa Na;
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI
TANESCO – MAKAO MAKUU, DODOMA

Leave A Reply