The House of Favourite Newspapers

TANESCO Watoa Tamko Kukatika kwa umeme Uwanja wa Benjamin Mkapa

0

Kufuatia kukatika kwa umeme Uwanja wa Benjamin Mkapa wakati mechi kati ya Yanga na Rivers United ya Nigeria ikiendelea, Shirika la Umeme Tanesco limetoa tamko.

Tamko hilo linasomeka kama ifuatavyo:

Uwanja wa Taifa una hudumiwa na vyanzo viwili vya Umeme. TANESCO na Majenereta ya uwanja.

Mechi ya leo uwanja ulikuwa unahudumiwa na Majenereta ya uwanja.

Baada Majenereta kushindwa kufanya Kazi katikati ya mchezo na taa kuzimika uwanja uliamua kutumia chanzo cha TANESCO na mchezo ukaendelea.

Tunasikitika kwa kadhia iliyo iliyo jitokeza na tutashirikiana na wenzetu kwa siku za usoni jambo hili lisijirudie.

RAGE ASHINDWA KUZUNGUMZA, AKIRI – ”YANGA SASA HIVI WANA TIMU MZURI, WANASTAHILI KUFIKA WALIPOFIKA”

Leave A Reply