The House of Favourite Newspapers

TANESCO Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Hitilafu ya Umeme Iliyojitokeza leo

0

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa ufafanuzi umma kuhusu hitilafu ya umeme iliyojitokeza leo Desemba 8, 2023 majira ya saa 04:14 asubuhi na kupelekea mikoa inayopata umeme kutoka katika Gridi ya Taifa kukosa umeme.

Taarifa ya TANESCO kwa umma imebainisha kuwa hitilafu hiyo imetokana na nguzo kubwa za kusafirisha umeme kutoka katika Kituo cha kuzalisha umeme kwa gesi asilia cha Ubungo III eneo la Mto Gide, Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam kusombwa na maji kupelekea hitilafu kutoka kwenye Gridi ya Taifa.

TANESCO imesema kwa sasa umeme umeanza kurejea kwa awamu katika mikoa iliyokuwa inakosa umeme na jitihada zinaendelea kuhakikisha mikoa yote inapata umeme mapema iwezekanavyo.

Aidha, jitihadi nyingine zinazofanywa na Shirika ni kuhakikisha miundombinu iliyoharibika inajengwa ndani ya muda mfupi, kuruhusu kusafirisha umeme unaokosekana katika Gridi ya Taifa kutoka Kituo cha kuzalisha umeme kwa gesi asilia cha Ubungo III.

“Shirika linawaomba radhi kwa kwa usumbufu uliojitokeza, na litaendelea kutoa taarifa za hali ya upatikanaji wa umeme kwa kadri hali itavyozidi kuimarika.” imesema taarifa hiyo.

Leave A Reply