The House of Favourite Newspapers

Tanga Cement Yasherehekea Miaka Ishirini Ya Udhamini wa Kilimarathon

0
Meneja Mkuu wa Biashara wa Tanga Cement PLC Peet Brits akigawa maji kwa baadhi ya wakimbiaji wa kilomita 42 na 21 waliokuwa wakipita kwenye kituo cha maji na soda cha Simba Cement wakati wa mbio za KiliMarathoni
SIMBA Cement imeendelea kuwa kinara wa ufadhili wa mbio za Kilimarathoni kwa miaka 20 sasa huku ikielezwa kuwa  mbio hizo za kimataifa zimezidi kuboreka zaidi kila mwaka.
Akizungumza mara baada ya kumaliza kwa mbio hizo zilizofanyika Februari 26, katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Meneja wa Biashara wa Tanga Cement PLC Peet Brits amesema, huu ni mwaka wa 20 wa ushiriki wao wakiwa wadhamini wakongwe na wakimbiaji kupitia timu za Simba katika mbio hizo ambazo Simba Cement na waandaaji wa Kilimarathoni wamekuwa wakiziboresha hadi kufikia miaka 21 kwa mwaka 2023.
Mkurugenzi Mtendaji  wa  Tanga Cement PLC Reinhardt Swart, (kulia)  akigawa maji kwa baadhi ya wakimbiaji wa kilomita 42 na 21 waliokuwa wakipita kwenye kituo cha maji na soda cha Simba Cement wakati wa mbio za KiliMarathoni
Amesema, udhamini wa mbio hizo ni kutokana na umuhimu wa michezo hasa Kilimarathoni ambayo huwakutanisha wafanyakazi wa Simba Cement na kufanya shughuli hii kwa umoja kama wanavyofanya viwandani pamoja kukutana na wadau pamoja na wateja wao.
“Katika ushiriki wetu hatukuangalia vyeo au nafasi zetu za kazi tuliona, Mkurugenzi Mtendaji akigawa maji kwa wakimbiaji…tulizungumza lugha moja kutoka langoni hadi kileleni kwa ushirikiano na wafanyakazi ambao ni wakimbiaji (Timu Simba,) kwa pamoja na wakimbiaji wengine, wadau na wateja.” Amesema.
Pia amesema, wakati wa baada ya mbio hizo wafanyakazi ambao ni wakimbiaji wamekutana na wateja na wadau wao Kanda ya Kaskazini  na kubadilishana mawazo ya uboreshaji katika huduma.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa  Tanga Cement PLC Mtanga Noor (kulia), akihudumia vinywaji kwa baadhi ya wakimbiaji wa kilomita 42 na 21 waliokuwa wakipita kwenye kituo cha maji na soda cha Simba Cement wakati wa mbio za KiliMarathoni zilizofanyika Moshi mwishoni mwa wiki
Kuhusiana na mafanikio kupitia mbio za Kilimarathoni Peet amesema, wamefurahi kushirikiana katika mbio hizo zilizofanyika kwa mara ya 21 sasa na kufanya vizuri katika mbio hizo pamoja na kutoa huduma ya kugawa maji kwa  wakimbiaji wa Kilometa 42 na 21 waliopita katika kituo chao cha kugawa maji.
 “Tuna uhakika wakimbiaji wamefurahi kupita katika kituo chetu cha Point 8 wakati wa mbio hizi na kupata huduma, tutaendelea kushiriki katika tukio hili kila mwaka… Tunaipenda na kuithamini Kilimarathoni na tunafurahi kudhamini kwa kugawa maji kwa wateja wetu na wadau wote waliopita katika ‘Water Point’ yetu na hawa ni kutoka katika mikoa ya Kaskazini ikiwemo Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga na mikoa mingine.” Ameeleza.
Aidha amesema, kwa mwaka huu walijipanga  kufanya vyema zaidi ikilinganishwa na mwaka uliopita kwa kuongeza idadi ya wakimbiaji kwa timu Simba pamoja na kuongeza nguvu baina yao kwa  kuwapa moyo wakimbiaji na kumaliza kwa ushindi.
Vilevile amesema, wamekuwa na Timu hiyo inayojumuisha wafanyakazi si kwa mashindano ya Kilimarathoni pekee na kampuni ilihakikisha gharama zote ikiwemo vifaa, malazi, usafiri na burudani zinatolewa kwa kila mshiriki ili waweze  kupata ushindi na kueleza kuwa wamekuwa na mashindano mbalimbali katika idara ambayo yameleta chachu kwa kampuni kudhamini timu hiyo ya Simba.
Peet amesema, kwa mwaka huu mwaka huu wamevenja rekodi kwa kuwa na jumla ya washiriki 28 na kupitia Kilimarathoni wamesherehekea kwa upekee mafanikio ya mwaka 2022 wakiwa washindi wa jumla wa tuzo ya Rais kwa mzalishaji  bora wa mwaka na mshindi wa jumla wa tuzo ya taarifa ya fedha iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu  na wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA.)
Leave A Reply