The House of Favourite Newspapers

Watuhumiwa 2,000 wa Ujambazi wa Kutumia Silaha Wahamishwa Kwenda Gereza Jipya

0

 

Serikali ya Salvador, imewahamisha watuhumiwa wa ujambazi wapatao 2,000 kwenda katika gereza jipya na kubwa lenye uwezo wa kuchukua wafungwa 40,000 kwa wakati mmoja.

Katika video inayosambaa kwa kasi kubwa mitandaoni, kundi kubwa la watuhumiwa wa ujambazi wa kutumia silaha, wanaonekana wakiwa wamedhibitiwa kikamilifu na askari wenye silaha, wakiwa wamenyolewa nywele na kuvalishwa kaptura huku miili yao ikiwa na tattoo nyingi.

 

 

“Haya ndiyo yatakayokuwa makazi yao mapya, mahali ambapo hawatakuwa na uwezo wa kuwadhuru raia tena,” ameandika rais wa nchi hiyo, Nayib Bukele kupitia akaunti yake ya Twitter.

Kwa kipindi kirefu, El Salvador ilikuwa ikitisha kutokana na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha na mauaji yanayosababishwa na biashara ya dawa za kulevya iliyoshamiri, ambapo mwaka mmpja uliopita, Machi 2022, Rais Bukele alitangaza hali ya hatari na mkakati maalum wa kumaliza uhalifu ambao ulikuwa umekithiri.

 

 

Tangu kuanza kwa mpango huo, maelfu ya watuhumiwa wa ujambazi wa kutumia silaha na biashara ya madawa ya kulevya, wamekamatwa huku wengine wakiuawa na kwa kiasi kikubwa, amani nautulivu vimerejea katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

Leave A Reply