The House of Favourite Newspapers

Tanzia: Kamanda Kidavashari Afariki Dunia

0

 

NAIBU Kamishna wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, Zahir Kidavashari,  amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne, Novemba 17, 2020 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya DCMC Ntyuka jijini Dodoma.

Kidavashari aliwahi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya.

Akizungumza na Global Digital, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, SACP Gilles Muroto amethibitisha kutokea kwa msiba huo.

“Taarifa za msiba huo ni za kweli, Kidavashari amefariki dunia.” 

 

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa pia na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro. Msemaji wa Polisi, David Misime amesema, alilazwa tangu Novemba 15 na ataagwa kesho kisha mwili wake utasafirishwa Arusha kwa maziko

Taarifa zaidi tutakueleta….

Leave A Reply