The House of Favourite Newspapers

Tantrade na Ubalozi wa Misri Kuandaa Mikutano Ya B2B Katika Sekta ya Hotel na Vifaa Vya Nyumbani

0
Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa Khamis leo tarehe 20 Juni, 2023 katika ofisi za TanTrade amekutana na Maafisa kutoka Ubalozi wa Misri nchini Ukiongozwa na Ndugu Mohammad Ally Atteya na Bi. Leila Adel, ambapo wamezungumzia maandalizi ya Maonesho na Mikutano ya B2B katika sekta ya Hotel na Vifaa vya nyumbani  kutoka Misri.
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika tarehe 17-19 Julai, 2023, Zanzibar ambapo Kampuni takriban 15 za Misri kwenye Sekta ya Utalii zitashiriki.
Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa Khamis amesema TanTrade itashirikiana na Ubalozi wa Misri katika uratibu kwa kutoa wataalam  kutoka TanTrade Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano huo.
Katika Mkutano  huo kutakuwa na Maonesho madogo ya Bidhaa pamoja na mikutano baina ya wafanyabiashara (B2B) wa Tanzania Misri.
Pamoja na kuwahakikishia ushirikiano, Mkurugenzi Mkuu aliwakaribisha kutembelea Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba yanayotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 28 Juni -13 July, 2023 katika Uwanja wa Mwl. J. K. Nyerere.
Leave A Reply