The House of Favourite Newspapers

TFF Yatoa onyo kali kwa Wanaoshirikiana na Wadau Waliofungiwa

0
Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Cliford Mario Ndimbo

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawakumbusha wanafamilia ya mpira wa miguu kuwa ni kosa kushirikiana na wadau ambao wamefungiwa.

Ni muhimu kuzingatia kuwa wadau husika wamefungiwa baada ya kwenda kinyume na Katiba, Kanuni na taratibu zinazosimamia mpira wa miguu.

Hivyo, TFF inaendelea kufuatilla ukiukaji huo ili kuchukua hatua stahiki.

Wanafamilia wote wanao wajibu wa kuheshimu Katiba, kanuni na taratibu zinazotawala mpira wa miguu.

Pia waliofungiwa wanajiweka katika hatari ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu iwapo hawatatumikia adhabu zao kikamilifu.

Leave A Reply