The House of Favourite Newspapers

Tanzania Kuendeleza Ushirikiano na India – Kassim Majaliwa

0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Magembe akizungumza na Wahariri na Wanahabari waandamizi (hawapo pichani) kutoka vyombo mbalimbali vya habari katika semina ya mwaka 2017 iliyoandaliwa na TANAPA kwa wanatasinia hiyo ya habari. Mkutano huo unafanyika jijini Tanga.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Magembe amewapongeza waandishi wa habari kwa mchango wao kuendelea kutangaza utalii nchinikupitia vyombo vyao, na kuwaomba waendelee na uzalendo huo kwani kitendo hicho ni faida kwa taifa zima.

 

 

Mmoja wa wahariri, Absalom Kibanda akitoa neno la shukrani mara baada ya semina hiyo kufunguliwa.

 

Pongezi hiyo ameitoa leo jijini Tanga alipokuwa akifungua semina ya mwaka kwa wahariri na wanahabari waandamizi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA).

 

Sehemu ya washiriki wa Semina ya Wahariri na Wanahabari waandamizi kwa mwaka 2017 iliyoandaliwa na TANAPA.

Waziri Magembe amesema matokeo ya wanahabari kutumia kalamu zao kutangaza utalii yanajionesha wazi kwa ongezeko la idadi ya watalii kutoka nchi mbalimbali kutembelea hifadhi zetu.

 

Meneja Mawasiliano wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Pascal Shelutete akitoa maelezo kwa Wahariri na Wanahabari waandamizi (hawapo pichani) kutoka vyombo mbalimbali vya habari katika semina ya mwaka 2017 iliyoandaliwa na TANAPA kwa wanatasinia hiyo ya habari.

Aidha ameitaka TANAPA kuendelea kushirikiana na wanahabari kwa kufanya semina hizo kila mwaka ili kupata mrejesho juu ya kazi wanayoifanya, kwani vyombo vya habari ni fursa nzuri ya kutoa elimu kwa umma na kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na mamlaka hiyo.

 

Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbas (kulia) nje ya ukumbi mara baada ya kufunzuliwa kwa semina ya mwaka 2017 kwa wahariri na wanahabari waandamizi iliyoandaliwa na TANAPA.

Mkutano huo wa siku tatu ulioanza leo Julai 26 unatarajia kumalizika Julai 29, ambapo wanahabari watajifunza na kujadiliana masuala mbalimbali ya utalii na uhifadhi.

Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari.

 

Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari.

 

 

Leave A Reply