The House of Favourite Newspapers

Tanzania na Kenya Zaondoa Vikwazo vya Biashara

0

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo amewahamasisha wafanyabiashara wa Kitanzania kuendelea kufanya biashara na kwenda kuwekeza nchini Kenya kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo iliyopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki  na amewataka  kuwasiliana na Wizara iwapo kutakuwa na changamoto zozote.

 

Hayo ameyasema katika Mkutano wa tano (5) baina ya Tanzania na Kenya kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya biashara ikiwemo vikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiushuru (NTBs) baina ya nchi hizo uliofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29 Mei 2021 katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) jijini Arusha.

 

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo amewahamasisha wafanyabiashara wa Kitanzania kuendelea kufanya biashara na kwenda kuwekeza nchini Kenya kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo iliyopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki  na amewataka  kuwasiliana na Wizara iwapo kutakuwa na changamoto zozote.

 

Hayo ameyasema katika Mkutano wa tano (5) baina ya Tanzania na Kenya kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya biashara ikiwemo vikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiushuru (NTBs) baina ya nchi hizo uliofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29 Mei 2021 katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) jijini Arusha.

Katika mkutano huo Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Mkumbo ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano  huo  ambao ulijumuisha Waziri wa  Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji, Waziri wa Kilimo, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, wakati  ujumbe wa kenya ukiongozwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Maendeleo ya Wajasiliamali Mhe. Betty Maina aliyeambana na Balonzi wa Kenya nchini Tanania.

 

Aidha, Waziri amesema kuwa mkutano huo ni utekelezaji wa maelekezo ya kuimarisha mahusiano ya biashara na nchi jirani yaliyotolewa katika ziara ya Kiserikali iliyofanywa nchini Kenya na, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 4-5 Mei 2021.

 

Prof. Mkumbo amesema mkutano huo wa kibiashara baina ya nchi hizo ulilenga kujadili masuala mbalimbali ya biashara katika sekta za kilimo, forodha, uhamiaji na usafirishaji.

Jumla ya masuala 64 yamejadiliwa ambapo kati ya hayo masuala 30 yametatuliwa na mengine 34 yaliyobaki yamewekewa mkakati maalum na muda wa utekelezaji.

“Miongoni mwa masuala yaliyotatuliwa kwa upande wa Tanzania ni pamoja na kuwezesha upitishaji wa bidhaa mpakani, hususan vinywaji baridi kama vile juisi kutoka Tanzania kwenda Kenya, kuondolewa kwa tozo za ukaguzi (inspection fees)zilizokuwa zinatozwa na Mamlaka za Kenya kwenye bidhaa za Tanzania, ikiwemo unga wa ngano, zenye alama ya ubora kutoka Mamlaka husika Tanzania, kuwezesha upitishaji wa mahindi kutoka Tanzania kwenda Kenya na Kuondoa ushuru wa asilimia 25 kwenye bidhaa za kioo kutoka Tanzania kwenda Kenya”  Prof. Mkumbo.

 

Kwa upande wa Kenya, masuala yaliyotatuliwa ni pamoja na kutoa upendeleo kwa bidhaa za sementi zinazozalishwa nchini Kenya ambazo zinakidhi matakwa ya vigezo vya uasili wa bidhaa vya na Jumuiya ya Afrika Mashariki, kutoa upendeleo maalum kwa vinywaji kutoka Kenya ikiwemo juisi za nanasi(Pineapple Juices) baada ya kukidhi vigezo vya uasili wa bidhaa vya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Leave A Reply