Tanzania Yafuzu Kucheza Afcon Nchini Ivory Coast, Yailazimisha Algeria 0-0
Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” chini ya kocha Adel Amrouche inafanikiwa kufuzu AFCON 2023, mara ya tatu kwenye historia dhidi ya Taifa la 33 kwenye FIFA Ranks, Tanzania “Underdogs” wakiwa 124 baada ya kuilazimisha Algeria matokeo ya 0-0
Tanzania ambayo ilishiriki AFCON Mwaka 1980 na 2019 imekamilisha michezo ya Kundi F ikiwa na pointi 8 nyuma ya Algeria yenye pointi 16 ambayo nayo imefuzu, Uganda ina pointi 7, Niger imeshika mkia kwa kuwa na pointi 2
Michuano hiyo inatarajiwa kufanyika Januari 13 hadi Februari 11, 2024 Nchini Ivory Coast
Mbinu za Amrouche kwenye mchezo huo wa kihistoria kwa Tanzania;
Mfumo
• Wakizuia 5-4-1
• Wakishambulia 3-4-3
Kikosi
• Beno Kakolanya (GK)
• Bakari Nondo (CB)
• Dickson Job (RCB)
• Ibrahim Baka (LCB)
• Haji Mnoga (RWB)
• Novatus Dismas (LWB)
• Sospeter Bajana (CM)
• Mzamiru Yassin (CM)
• Kibu Denis (RW)
• Simon Msuva (LW)
• Clement Mzize (CF)
Staili ya uchezaji
• Sanaa ya uzuiaji
– Stars walifanya analysis nzuri kwa Algeria na kuja na mpango sahihi wa kuzuia kwa kuwa nyuma ya mpira na kuwaachia Algeria muda na nafasi wakiwa mpira kwenye theluthi zao mbili za mwanzo (Build up phase & Middle Phase)
Stars walibana theluthi zao mbili za mwanzo (Mid & Low Block) wakizuia na shinikizo la chini wakiwa pamoja na muundo wa 5-4-1, mistari ya uzuiaji ikiwa;
– 1st line Bakari, Job, na Baka huku pembeni yao kukiwa na Mnoga na Nova
– 2nd line, Bajana na Mzamiru mbele ya CB’s, Msuva na Kibu mbele ya WB’s
-3rd line, Mzize
Stars walizuia njia zote za Algeria
1. Katikati, Kibu alizuia mabeki na kiungo wa kati wa Algeria Zorgane/Remiz kupita katikati, Bajana na Mzamiru walizuia nafasi mbele ya CB’s isiweze kuwa wazi kwa viungo washambuliaji wa Algeria Abdelli na Kadri kuli-dormibate ( Zone 14)
2. Pembeni, Msuva na Kibu wali-track mikimbio ya Full-backs wa Algeria, Kerkhof na Nouri waki-overlap pembeni ili ukuta wa Stars isitanuliwe na Nova na Mnoga kujikuta 2v1
3. Job na Baka wali-mark vyema washambuliaji wa pembeni wa Algeria Bouanani na Chaibi wakiingia kwenye half-space
3. Bakari alikua Sweeper/Libero kusafisha na kusaidiana na wenzake kucheza mipira ya juu
• Kushambulia kimkakati
Stars walitumia mashambulizi ya moja kwa moja kwenye muundo wa 3-4-3
– Mnoga na Nova husogea pembeni ya Mzamiru na Bajana
– Msuva na Kibu husogea usawa wa Mzize
Walishambulia zaidi kwa kujibu, nyakati Algeria hawa-regain shape.
STORI NA SISTINHO,GLOBAL RADIO, CHAMPIONI