The House of Favourite Newspapers

Tanzania Yapanda Viwango Vya FIFA

0

TANZANIA  imepanda kwa nafasi tatu katika viwango vya ubora wa soka vya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kwa mwezi Septemba.

 

 

Kwa mujibu wa viwango vipya vilivyotangazwa leo Septemba 16, Tanzania imepanda kutoka nafasi ya 135 hadi ya 132 na kuzipiku nchi za Togo, Lithuania na Comoro ambazo zilikuwa juu yake katika viwango vya ubora vya mwezi uliopita.

 

Kwenye mechi za hivi karibuni Taifa Stars imefanikiwa kutoa sare na DRC  ya mabao 1-1 na kisha kuichapa Madagascar kwa mabao 3-2 zikiwa ni mechi za kufuzu kuwania fainali za kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

Leave A Reply