The House of Favourite Newspapers

Kumbe, Kabwe Afia Alipofia Adam Kuambiana

0

kabweMarehemu Wilson Kabwe.

MKURUGENZI wa zamani wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe aliyesimamishwa kazi na Rais John Magufuli, Aprili 19 mwaka huu amefariki usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam.

Chanzo cha uhakika kimeuambia mtandao huu kwamba Kabwe alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hivi karibuni, alisafirishwa kwenda India kwa matibabu. Aliporejea nyumbani, ndipo siku chache baadaye, akakutana na dhoruba ya kikazi.

Ingawa haijatajwa ugonjwa wake, lakini watu walio karibu na familia yake wanadai alikuwa akisumbuliwa na kiharusi (Stroke). Akiendelea na matibabu akiwa nyumbani, hali yake ilibadilika ghafla siku nne zilizopita na familia yake ikamkimbiza katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge ambako alilazwa na kupatiwa matibabu.

kabwe, meya na madiwani mwanzaAliyekuwa Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe (wa nne kutoka kushoto), aliyekuwa Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (wa tatu kutoka kushoto ambaye kwa sasa ni Mbunge wa jimbo la Nyamagana) wakiwa na baadhi ya madiwani na wakuu wa idara wa jiji la Mwanza.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amethibitisha kifo hicho na habari zinasema msiba upo nyumbani kwake, Uganda Avenue Masaki, jijini Dar es Salaam. Taarifa kutoka msibani hapo zinasema taratibu za mazishi zinaendelea na kwamba marehemu ataagwa siku ya Jumanne na kusafirishwa siku hiyo hiyo kwenda kwao, Same mkoani Kilimanjaro ambako atazikwa kesho yake, Jumatano.

Kabwe alisimamishwa kazi na Rais John Magufuli wakati wa ufunguzi wa Daraja la Mwalimu Nyerere (Kigamboni) kufuatia madai ya kutofuata taratibu za utumishi zilizotolewa na Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Tuhuma dhidi yake zilihusu madai ya ufisadi katika utekelezaji wa mikataba inayohusu maeneo ya ukusanyaji mapato katika Stendi Kuu ya mabasi yaendayo mikoani (Ubungo Terminal) na kodi ya uegeshaji magari katika Jiji la Dar es Salaam hivyo kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. 3 Bilioni.

JPM_Rais

Rais John Magufuli akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Daraja NSSF Kigamboni ambalo limepewa jina jipya na kuitwa Daraja la Nyerere, jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Picha na Anthony Siame

Rais Magufuli alichukukua uamuzi huo siku ya uzinduzi wa daraja la Kigamboni, ambapo kabla ya Rais kuhutubia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda alitoa hotuba fupi ya maswala kadhaa ya Mkoa wa Dar es Salaam  ikiwemo  ripoti ya tume aliyounda  kuchunguza utekelezwaji wa mikataba hiyo.

Kabla ya kuhamishiwa jijini Dar es Salaam, Kabwe alikuwa ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza ambaye alihamishiwa Mwanza akitokea Mbeya baada ya kutuhumiwa kwa  ufisadi wa mabilioni kadhaa jijini humo.

Hadi mauti yanamkuta, Kabwe ambaye ni msomi mwenye Digrii ya kwanza ya sheria (LL.B) aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alikuwa ni mmoja wa maofisa waandamizi katika Tamisemi, akiwa ametumikia kwa zaidi ya miaka 13, akiongoza Halmashauri tatu za Mbeya, Mwanza na Dar es Salaam.

SAM_2067Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza (wakati huo), Wilson Kabwe akipokea msaada wa madawati kutoka kwa aliyekuwa mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (Picha na MAktaba).

BAADHI YA MATUKIO YANAYOMHUSU

Akiwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, mwaka 2010 ndiye aliyeibua hoja kuwa Mbunge wa zamani wa Nyamagana, Ezekiel Wenje kuwa hakuwa raia wa Tanzania, hoja ambayo hata hivyo ilishindwa.

Mei 11, 2013 aliteuliwa na aliyekuwa Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia kuwa Mkurugenzi Jiji la Dar es Salaam, nafasi aliyodumu nayo hadi April 19, aliposimamishwa kazi kwa tuhuma zilizotajwa hapo juu. Hata hivyo, Rais Magufuli siku hiyo alisema, hana matatizo na Kabwe kama vyombo husika vitamsafisha.

kuambiana4Marehemu Adam Kuambiana

Adam Kuambiana, aliyekuwa muongozaji na muigizaji wa filamu Tanzania, aliyefariki dunia miaka miwili iliyopita, aliaga dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo pia.

VIDEO: RAIS MAGUFULI ALIVYOMSIMAMISHA KAZI WILSON KABWE

VIDEO YA WENJE ALIVYOMWANIKA KABWE BUNGENI

Leave A Reply