The House of Favourite Newspapers

TANZIA – Mfanyabiashara Haroon Zakaria Afariki Dunia

0
Mfanyabiashara mkubwa na bilionea wa Kitanzania, Haroon Zakaria enzi za uhai wake.

MFANYABIASHARA mkubwa na bilionea wa Kitanzania, Haroon Zakaria amefariki dunia hii leo Mei 1, 2021. Zakaria ndio Mmiliki wa Makampuni kadhaa ikiwemo Murzah Oil mills, Zan Fast Ferries na Majipoa.

 

Kampuni ya Murzah Oils ndiyo iliyompatia umaarufu zaidi Zakaria, ambayo ilianzishwa mwaka 1997 ikiwa inazalisha bidhaa mbalimbali zinazoongoza Afrika Mashariki, ikiwemo mafuta ya kula ya Korie, Sun Drop na mengineyo, sabuni zikiwemo Foma na Kiboko sambamba na bidhaa nyingine za usafi.


Pia viwanda vyake vilivyopo chini ya Murzah Group of Companies, vilikuwa vikizalisha bidhaa mbalimbali za vyakula, ukiwemo mchele, unga wa ngano na kadhalika ambazo zilikuwa zikiuzwa ndani na nje ya nchi.

 

Zakaria alikuwa ni miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wa sukari kwa kipindi kirefu, akiwa na duka kubwa eneo la Kitumbini, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa akiagiza sukari kutoka nje ya nchi na kuiuza kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa.

 

Amewahi kuingia katika mgogoro na serikali, kwa kudaiwa kuhodhi kiasi kikubwa cha sukari na kusababisha uhaba nchi nzima, kisha shehena za zaidi ya tani nne na nusu ikakutwa kwenye maghala yake, jambo ambalo baadaye lilimalizwa kwa mazungumzo na serikali.

 

Zakaria atakumbukwa kwa moyo wa upendo aliokuwa nao, ambapo aliwasaidia wafanyabiashara wadogo mitaji pamoja na kuwasafirisha nje ya nchi watu mbalimbali waliokuwa wakihitaji matibabu ya kitaalamu ambayo hayakuwa yakipatikana nchini.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Leave A Reply