The House of Favourite Newspapers

Tanzia: Mzee Yusuf Afiwa na Baba Yake Mzazi

0


MSANII mkongwe wa muziki wa taarab nchini, amepata pigo la kuondokewa na baba yake mzazi, Yusuf Mzee,  kilichotokea leo, Jumanne Februari 2, 2021, Fuoni visiwani Zanzibar.

 

Mzee Yusuf amethibitisha taarifa hizo na kueleza kwamba baba yake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa homa ya matumbo (typhoid) ambapo alipelekwa hospitali na kutibiwa kisha kuruhusiwa lakini ghafla hali ilibadilika na kupoteza maisha.

 

Kwa mujibu wa Mzee Yusuf, mazishi yanatarajiwa kufanyika hapo kesho, Februari 3 katika makaburi ya Fuoni, Zanzibar.

Leave A Reply