The House of Favourite Newspapers

Taratibu Mazishi ya Mtangazaji Mukhsin Mambo

0

MWANDISHI wa habari, Mukhsin Mambo, aliyefariki dunia jana Februari 8, 2021,  akiwa nyumbani kwake nchini Marekani, anategemewa kuzikwa jijini Mwanza maeneo ya Capri Point kwa dada yake.

 

Hayo yameelezwa na Bernard James ambaye ni mmoja wa watu aliowahi kufanya nao katika vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.

 

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa taarifa za awali, Mambo, alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa kipindi cha muda mfupi na kwamba mpaka mauti yanamfika alikuwa anajisikia vibaya kabla ya kukimbizwa hospitali.

 

Mukhsin Mambo amewahi kufanya kazi katika kituo cha Radio Free Africa (RFA) Mwanza na TV1.

Leave A Reply