The House of Favourite Newspapers

Tarimba Atoa Tamko Zito kwa Masikitiko, Awatakia Simba Kila Lakheri

0
Tarimba Abbas Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SportPesa

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa SportPesa, Tarimba Abbas, amewatakia heri Klabu ya Simba kwa kuingia mkataba mpya na M-Bet, huku akiwashukuru kwa ushirikiano wao ndani ya miaka mitano ya udhamini wao.

 

Tarimba amesema ulikuwa mkataba wa mafanikio makubwa, hivyo baada ya kupata barua yao ya kuachana nao rasmi walifurahi maana wana mengi ya kujivunia kutoka kwao ikiwa ni pamoja na mafanikio walioyafikia Simba katika soka.

Tarimba Abbas

Sportpesa amekuwa mdhamini wa vilabu vyote viwili vikubwa nchini Tanzania vya Simba na Yanga, kitendo Simba kusaini mkataba mpya na M- Bet ni ishara tosha kuwa Sportpesa anaweza kubaki kuwa mdhamini wa klabu ya Yanga kama atafanikiwa kusaini mkataba mpya na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya NBC.

Leave A Reply