The House of Favourite Newspapers

Tatizo la uzazi kwa wanaume ‘Male Sterility’

infertility_maleinfertility_treatmentTatizo hili  husababisha  mwanaume  kushindwa  kumpa  mwanamke   mimba   ambapo  hutoa  mbegu zisizo  na  sifa  kurutubisha  mayai  ya  mwanamke  au  kushindwa  kabisa  kutoa  mbegu  hizo.

CHANZO CHA TATIZO

Hali  ya  mwanaume  kushindwa kusababisha  ujauzito  kitaalamu  tunaita  ‘Failure to Impregnate’  ambayo husababishwa na  mambo  mbalimbali  yanayoathiri  utendaji  kazi  wa  mfumo  wa  mwili   na uzazi.

Athari  hizo husababisha mwanaume  atoe  mbegu  za  kiume  zisizo  na sifa. Matatizo  ya  kutokutoa mbegu  yanatokana na athari katika kiwanda cha uzalishaji  mbegu  au korodani. Mbegu zinaweza zisitoke kutokana  na njia yake kuziba au zisifike ukeni,  yaani  zisitoke au zitoke kwa kiasi  kidogo  sana.

Kiwanda  cha  uzalishaji  mbegu  kushindwa  kufanya  kazi  vizuri husababishwa  na  kuumia korodani, maambukizi  sugu mfano  magonjwa  ya  zinaa, kifua  kikuu na  joto  kali.  Kusinyaa kwa  korodani  yaani kuwa ndogo  sana, kupotea  kwa  korodani  ambapo  mwanaume  hana  kabisa  korodani na  magonjwa mengine  yanayoathiri  mfumo  wa  homoni  mwilini. Magonjwa   sugu  kama  kisukari, kansa  na  HIV  pia  huchangia  hali hii. Lishe  mbovu  kwa  kutokula  vizuri  kutokana  na  kukosa  chakula,  matumizi  ya madawa  ya  kulevya  na  ulevi  wa   pombe  ambapo  mtu  hupoteza  hamu  ya  kula pia huchangia.

Mionzi  ya  mara kwa  mara  mfano  X-Ray  au  mionzi  ya  viwandani, matumizi  makubwa ya dawa  za homoni  kwa lengo  la  kuongeza  nguvu  bila  utaratibu maalumu pia huweza kuchangia.

 Chanzo  cha  pili  ni  kuziba  kwa  njia  za  kupitisha  mbegu  ambapo  husababishwa  na maambukizi, upasuaji  katika  maeneo  ya   korodani au  henia  na  kujikuta  unaharibu  njia  za  kupitisha  mbegu, kuumia  korodani,  matatizo  ya  njia  ya  mkojo  na  tezi dume.

Chanzo  cha  tatu  ni  kushindwa  kufanya  tendo  la  ndoa  kutokana  na  kutokuwa  na  nguvu  za kutosha  au  kukosa   kabisa nguvu  za  kiume.  Hali  hii  huwa  na  vyanzo  mbalimbali  kama tulivyozungumzia  katika  matoleo  yaliyopita.

Lakini  kasoro  za  uume  na  kuwahi  kumaliza  tendo  la  ndoa pia  huchangia.

DALILI ZA TATIZO

Mwanaume  mwenye  tatizo  la uzazi  huwa  na  dalili  mbalimbali,  mojawapo  ya  dalili  hizo  ambazo moja  kwa  moja  ni  viashiria  vya  kuwa  na  tatizo ni  kama  vile  kutotoa  kabisa  manii  wakati  wa tendo.

Pia maumivu  ya  njia ya mkojo na mkojo kutotoka vizuri mara kwa mara, kasoro za kimaumbile katika uume au korodani, kuondolewa tezi dume, kutoa manii lakini zikakosa mbegu, kutoa mbegu chache zisizokidhi kiwango.

Matatizo ya mbegu  huwa  yanagunduliwa  hospitali  baada  ya  uchunguzi wa kina. Kuhusu maambukizi ya mara kwa mara ya njia  ya  mkojo  kwa mwanaume inashauriwa pia na mwenzi wako atibiwe, vinginevyo  naye atapatwa na maambukizi ya mara kwa mara ukeni.

UCHUNGUZI

Mwanaume  mwenye  tatizo  la  uzazi  ana  historia  ya  kukaa  na  mwanamke  kwa  angalau  mwaka mmoja wanatafuta  mtoto  lakini  hawapati. Mwanaume   ataanza  kuonyesha  dalili  kama  tulizozieleza  au  asiwe  nazo. Tatizo hili  la uzazi kwa  mwanaume  halijalishi  kama  tayari  una  watoto  au  huna tatizo  katika  ufanyaji  wa  tendo  la  ndoa.

Vipimo  mbalimbali  vitafanyika  kwa daktari  bingwa  wa  matatizo  ya uzazi  katika  hospitali  kubwa  za mikoa.

MATIBABU

Baada ya uchunguzi wa kina ambapo mwanaume atapimwa mkojo, vipimo vya damu huangalia vichocheo na maambukizi, pia mhusika atapimwa manii kuangalia matatizo mbalimbali pamoja na sifa za mbegu za  kiume  kama  zipo.  Vipimo na tiba  itategemea  matokeo  na jinsi daktari  atakavyopanga.

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.