TAWA Yawaonya Watoto, Wazee Na Wajawazito Marufuku Kufukuza Tembo
Morogoro, 18 Mei 2023: Mamlaka ya Usimamizi Wanyama Pori Tanzania (TAWA) imetoa tahadhari kwa wananchi wanaopakana na mapori ya akiba pamoja na hifadhi kuacha kutembea usiku kama hakuna ulazima ili kuondokana na madhara ya kushambuliwa na wanyama.
Ni kikao maalum kujadili utatuzi wa changamoto ya muda mrefu wanyama wakali na waharibifu kama vile Tembo katika wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wanaotoka maeneo ya hifadhi na kuingia kwenye maeneo ya shughuli za kibinadamu wakisababisha uharibu wa mazao mashambani pia baadhi ya watu kujeruhiwa na wengine kupoteza maisha.
Imesisitizwa kuwa watoto, wajawazito na wazee wasijiusishe kabisa katika zoezi la kuwafukuza Tembo kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha usalama wao.
Mlage Kabange ni Kaimu Naibu Kamishna wa Uhifadhi TAWA anasema kinachoendelea sasa ni mipango mikakati ya kukabiliana na wanyama waharibifu kuanza kutoa elimu kwa jamii kujilinda wao wenyewe na mali zao.
HABARI/PICHA NA MWAJUMA RAMBO/ GPL Morogoro.