The House of Favourite Newspapers

TAWCA, kusaidia wanawake wahasibu nchini

0

1.

Mwanachama mwanzilishi wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu, Anna Shanalingigwa (kushoto anayezungumza), akiwa na makamu wake, Neema Kiure, na Mratibu wa taasisi hiyo, Rose Majuva.

2.Makamu Mwenyekiti wa TAWCA,Neema Kiure Mssusa,(katikati) akionesha cheti chao taasisi yao.

Neema Kiure Mssusa (katikati) akionesha cheti chao cha usajili wa taasisi hiyo.

3.Mkutano ukiendelea.

Mkutano ukiendelea.

4.Wanahabari wakichukua tukio.Wanahabari wakichukua matukio.

TAASISI ya Wanawake Wahasibu Tanzania ijulikanayo kama ‘Tawca’ (Tanzania Association of Women Certified Accountants) imepanga kuwasidia wanawake wahasibu na wakaguzi wa hesabu kufikia malengo yao ya kitaalamu.
Akizungumza leo na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa TAWCA, Bahati Geuzye, amesema kuwa taasisi yao imesajiliwa rasmi na msajili wa taasisi zisizokuwa za kiserikali katika Wizara ya Mambo ya Ndani chini ya sheria ya uandikishwaji wa taasisi Agosti 5 mwaka huu na kufanikiwa kutunukiwa cheti cha usajili chenye namba S.A 20210.
Bi Bahati amesema kuwa TAWCA imeanzishwa chini ya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu, Tanzania (NBAA) ili kukidhi mahitaji ya wanawake wahasibu na wakaguzi kwa kupitia ushirikiano katika masuala ya kielimu, utandawazi, uongozi na shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa kuongozwa na katiba yake.
Amesema kuwa taasisi hiyo pia itaweza kusaidia wanawake na wasichana ambao wana malengo ya kuwa wahasibu wenye taaluma kwa kujiunga kwenye kozi mabalimbali zinazotolewa na Bodi ya Wahasibu na wakaguzi nchini.
Aidha mwenyekiti huyo amesema wanachama wa taasisi hiyo watakuwa ni wanawake wenye vyeti vya uhasibu vinavyotolewa na Bodi kwa ngazi zote kama vile, Graduate Accountant (GA) Associate and Fellow Certified Public Accountants (ACPA) pamoja na Associate and Fellow Certified Accountants in Public Practice (ACPA-PPs and FCPA-PPs) hivyo akiongeza kuwa watakuwepo wanachama wa heshima (Honorary members).
Hata hivyo Bahati amesema TAWCA inatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho Oktoba 6 mwaka huu kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam,
huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Servacius B. Likwelile.
Picha/Habari : DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply