The House of Favourite Newspapers

Tawi la Mpira pesa wapigana makonde

img_0090

WANACHAMA wa Klabu ya Simba, Tawi la Mpira Pesa la Magomeni jijini Dar leo walifikia hatua ya kukunjana mashati na kurushiana makonde kufuatia  kushindwa  kuelewana.

img_0078

Wapenzi wa Simba wakitaharuki vurugu hizo.

img_0076

img_0061
Tawi la Mpira Pesa linaloongozwa na mwenyekiti wake, Ostadhi Masoud, walifikia hatua hiyo kwa kile kilichodaiwa kutakiwa kuhama katika nyumba waliyopanga kutokana na kukiuka baadhi ya masharti ya kimkataba.
Akizungumza na mtandao huu, mwenyekiti wa tawi hilo, Ostadh Masoud alisema kuwa: “Tuliambiwa tuhame hapa tangu Agosti mwaka jana kutokana na baadhi yetu kukiuka masharti ya kimkataba, sasa leo (jana) tulikuja kwa nia ya kuhamisha vitu lakini wenzetu wakawa wanagoma ndiyo ikatoa hali hii kushikana mashati na kurushiana ngumi.

Comments are closed.