The House of Favourite Newspapers

TAXIFY YAWAWEZESHA MADEREVA WA BAJAJI KWA KUWAPATIA SIMU ZA SMARTPHONE

Kampuni ya Taxify inayokuwa kwa kasi zaidi duniani katika utoaji wa huduma ya usafiri kidijitali, sasa inawawezesha madereva-washirika wake wa Bajaji kwa kuwapatia simu za kisasa aina ya Smartphone.

Mpango mkakati huo umelenga kuwasaidia madereva wa Bajaji kutumia huduma ya Taxify kwa urahisi, kuboresha biashara na kujiongezea kipato cha juu zaidi.

Meneja Uendeshaji wa Taxify Tanzania, Remmy Eseka alisema,”Mamia ya madereva wa Bajaji wanatamani sana kufanya kazi pamoja nasi lakini changamoto kubwa inayowakabili ni kutokuwa na simu za kisasa yaani ‘Smartphones’. Tunarahisisha kwa madereva kutumia huduma mbalimbali za Taxify kwa kuwapatia vitendea kazi hivi kwa mkopo.

Kupitia mapato watakayokuwa wanapata mara baada ya kuanza kufanya kazi na sisi wataweza kulipia mikopo yao kidogo kidogo na kwa awamu.”

Kwa upande wake, dereva wa Bajaji ambaye ni mkazi wa Kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam, Steven Simon alisema, Taxify imeleta mabadiliko ya jinsi wanavyofanya biashara kwa sasa.

“Kupitia Taxify, sasa hatuna tena haja ya kusubiri kwa muda mrefu kusubiria wateja, tunaweza kupokea maombi ya wateja kutoka sehemu yoyote ya maeneo ya jijiji. Tumefanikiwa kupata kipato zaidi kuliko tulichokuwa tunapata hapo awali,” aliongeza.

Taxify imedhamiria kuwawezesha madereva wanaofanya nao kazi kujiongezea kipato. Kamisheni inayochukuliwa kwa kila safari ni asilimia 15 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 25 katika soko hilo la usafirishji kidijitali. Hii ina maanisha kwamba Taxify inatoza gharama ndogo za nauli kwa abiria wake huku madereva wakijipatia kipato kikubwa ukilinganisha na wadau wengine wanaotoa huduma ya usafiri kidijitali.

-Mwisho-

Comments are closed.