The House of Favourite Newspapers

TBA Yakiri Kubomoka kwa Mabweni Mapya ya UDSM Yaliyozinduliwa na JPM

0

MKURUGENZI wa Wakala wa Majengo nchini (TBA), Mhandisi Elius A. Mwakalinga, amekiri picha zinazosambaa mitandaoni zikionyesha majengo mapya ya mabweni ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM) yana nyufa ni za majengo hayo, huku akisema ni kitu cha kawaida kwa majengo makubwa.

Mwakalinga amesema kutokea kwa nyufa hizo ni moja ya hatua za ‘expansion joint’ ambazo hutumiwa kwenye ujenzi wa majengo, lakini majengo hayo yamekidhi vigezo vyote na vipimo wakati wa ujenzi wake.

 

“Kila design tunayofanya ya majengo sasa hivi tunatumia expansion joint, majengo mengi makubwa huwa inatumia hiyo, hivyo ni common na sio creck kubwa sana kama inavoonekana kwenye picha, nilienda ile jana usiku kukagua tukakuta hiyo hali, ni process za majengo ili yaweze kusatle, hivyo watu wawe na amani kabisa wala wasiwe na hofu”, amesema Bwana Mwakalinga.

 

Mwakalinga ameendelea kwa kusema kwamba watu wanaosambaza picha hizo bila kutaka ufafanuzi kutoka kwake wanafanya makosa kwani wanawatia watu hofu kwa jambo la kawaida kwenye hatua za ujenzi, huku wakilaumu kitu ambacho hawana uhakika nacho.

Majengo hayo yenye nyumba za makazi 644 yaliyojengwa na TBA kwa miezi minane yakielezwa kugharimu Sh10 bilioni yalizinduliwa Aprili 15, 2017 na Rais John Magufuli ambapo ujenzi ulifanyika ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais la kumaliza tatizo la malazi kwa wanafunzi wa UDSM.

 

CTREDIT: EATV

Leave A Reply