The House of Favourite Newspapers

TBBF Yatangaza Mashindano ya Mr. Tanzania na Mr. Photogenic

0
Mwenyekiti wa Chama cha Watunisha Misuli nchini (Tanzania Bodybuilding Federation  – TBBF) Chiwalalal akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).
Mwigizaji wa filamu, Mzee Chilo (kulia) akielezea jambo kwenye mkutanohuo akiwa  anatoka kwenye mmoja wa wadhamini wa mashindano hayo waitwao  Pilipiki Entertaiment.
Mdhamini wa mashindano hayo, Nilesh Bhatt,  akielezea walivyojizatiti kusaidia mashindano hayo.
Katibu Mkuu wa TBBF, Francis Mapungilo akizungumza.

CHAMA cha Watunisha Misuli nchini (Tanzania Bodybuilding Federation  -TBBF) imetangaza rasmi tarehe maalum ambayo itafanyika mashindano ya Mr.Tanzania, Style, Icon (Mr. Handsome na Mr. Photogenic, Desemba 16 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar, Katibu Mkuu wa TBBF, Francis Mapungilo, alisema kuwa pia mashindano hayo yatakuwa na ‘reality show’ kupitia televisheni ya Azam TV 2.

 

Katika kuelekea mashindano hayo kutakuwa na mchujo kuanzia Desemba 12 kwenye kambi maalum itakayokuwa imeandaliwa na  kutakuwa na semina maalum kwa majaji wa mashindano ya kutunishamisuli (bodybuilding).   Aidha ameeleza kuwa utaratibu utakaotumika katika upatikanaji wa tiketi utakuwa ni kwa njia ya mtandao na vituo maalum ambavyo vitatangazwa.

HABARI: DENIS MTIMA | GLOABAL PUBLISHERS

Breaking News: Polisi Yawakamata Waliovamia Ofisi za Mawakili wa Manji

Leave A Reply