The House of Favourite Newspapers

Tecno Camon 15, Simu Yenye Muonekano na Teknolojia ya Hali ya Juu

0

UBUNIFU zaidi wa teknolojia unaendelea kutenda haki duniani ambapo mawasiliano yanafanyika katika muda unaotakiwa na kikamilifu kuliko hapo mwanzo.

 

Teknolojia mbalimbali zimeleta mabadiliko ya haraka kutoka katika simu za kawaida za kuwapigia watu na kutuma ujumbe hadi simu za kisasa (smart phones).

Tanzania ina idadi kubwa ya watu wanaotumia simu za kisasa, hata hivyo wengi wao hukabiliwa na changamoto katika kupata simu zenye ubora wa hali ya juu na zenye bei bora.

 

Kampuni ya Tecno Mobile Tanzania ndiyo mkombozi kwani inajivunia utaalam wa kila aina wa bidhaa zake ambazo ni simu za kisasa zenye teknolojia ya hali ya juu ambazo Watanzania wanaweza kuzinunua.

 

Kampuni hiyo kubwa ambayo inafahamika kwa kutoa simu mbalimbali kama za Tecno Camon X, Camon 11, Camon 12, Camon 13 na zingine,  hivi sasa imetoa simu ya Camon 15.

 

Meneja Uhusiano wa Tecno Tanzania, Erick Mkomoya

Meneja Uhusiano wa Tecno Tanzania, Erick Mkomoya, amezungumza na mwandishi wa gazeti la Citizen kuelezea bidhaa hiyo mpya ya Camon 15.

 

Mkomoya anasema kimsingi Camon 15 ni muhimu kwa watu mbalimbali na inakidhi mahitaji yote muhimu ya kila siku ambayo ni pamoja na wafanyabiashara katika mitandao, waandishi wa habari, watalii, wanamitindo, wataalam wa usanifu na makundi mengine katika jamii.

 

Anaongeza kwamba, “Camon 15 ni mwendelezo zaidi wa kitaalam wa simu zilizopita, ina kila kitu cha kuhakikisha mteja anapata kila huduma aitakayo.

  1. Umbo la kuvutia

Camon 15 ina rangi ya kuvutia na maelekezo kamili ya matumizi yake.

  1. Taa maalum (Quad flashes)

Ina taa maalum nyuma yake ambazo zinafanya kazi kikamilifu katika mazingira ya giza na hutoa picha safi.

 

  • Picha ya 8x Ultra

Ina lensi ya 48MP na uwezo wa 8x wa kukuza picha.  Upigaji picha unanasa taswira nzuri ya kuvutia ambapo ubora wa picha hufikia asilimia 68%.

Pixels nne huunganishwa katika micron megapixel ya 1.6 ili kutoa picha za ubora wa kiwango cha juu.  Sensa kubwa ya 1/2” hunasa mwanga zaidi wakati wa usiku na kutoa picha zenye mwanga zaidi na isiyo na kelele.

CAMON 15, hunasa matukio zaidi nyakati za mchana na usiku.

  1. Upigaji picha za sentimita mbili

Upigaji picha za umbali wa sentimita mbili (close up shots) hukufanya kugundua ubora usioonekana wa vitu vidogo vilivyo kando yako.

  1. Ina kamera ya mbele ya 16 Mega pixels

Camon 15 ina kamera ya mbele yenye lensi ya 16MP kwa ajili ya kujipiga picha ambapo hutoa taswira iliyokamilika, yenye kuonekana vyema na mwanga wa kutosha.

  1. Uwezo wa betri

Betri ya 5000mAh hukupa kila ukitakacho katika kazi zako za kila siku na inauwezo wa kukaa na chaji kwa muda mrefu.

  • Inafunguliwa kwa kutumia sura (Face unlock)

Ina uwezo wa kutambua macho yako yaliyofumbwa, hivyo kukupa faragha na usalama katika simu yako.

 

Vitu vingine ni; flashi mbili za mbele, beautification, portrait bokeh effect, social turbo, dark theme, 64 GB space, fun social interaction, Dot-in display, artificial intelligence detection scene, super HDR, artificial intelligence body shaping, newly developed background.”

Simu hiyo ya utaalam wa kiwango  cha juu ya Camon 15 ilizinduliwa Aprili 20, 2020 jijini Dar es Salaam, ambapo mwigizaji maarufu wa Tanzania, Elizabeth Michael maarufu kama ‘Lulu’, alihusika.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Lulu alisema, Tecno ilifanya kazi kubwa na wakati sahihi katika kuzindua bidhaa hii akiamini ingekata kiu ya wapenda picha na tasnia ya filamu nchini akiwemo yeye.

 

“Inaeleweka wazi kamba picha huchukua nafasi kubwa katika maisha yetu; kila tunachofanya kila siku tunategemea picha hizi kutusaidia kuendeleza kazi zetu, hususan kutoka katika kamera zenye ubora wa hali ya juu.  Mimi mwenyewe naipenda Camon 15,” alisema Lulu.

Aliendelea kusema kwamba umbo na mwonekano wa simu hiyo ni baadhi ya mambo yaliyomvutia kuipenda.

 

Wakati wa hafla hiyo, Meneja Mauzo wa Tecno, Mariam Mohamed, alizindua promosheni  ya Camon 15 nchini kote akisema mteja ambaye angeinunua angezawadiwa begi la bure au kiboksi cha chakula au vyote viwili.

“Ofa hii iko nchini kote katika maduka yetu ya Tecno, hivyo wote mnakaribishwa,” alisisitiza.

 

Isitoshe, wakati huu ambapo dunia inapigana dhidi ya janga la Covid-19 ambapo kuna nchi ambazo watu hawatakiwi kutoka katika makazi yao na  kutokaribiana, Camon 15, inakuwezesha kupiga picha zenye mwanga mzuri na bora ukiwa katika umbali unaotakiwa, mchana na usiku.

 

 

 

Leave A Reply