The House of Favourite Newspapers

Tecno Camon 16s Kuingia Sokoni Hivi Karibuni

0
     Mwonekano wa mbele na nyuma wa TECNO CAMON 16s

Kampuni ya simu za mkononi ya TECNO inatarajia kuzindua simu mpya ya TECNO CAMON 16s, ni simu ambayo inakuja na teknolojia kubwa ya kamera na uwezo mkubwa  utakaowanufaisha watumiaji katika shughuli zao za kiofisi na kiuchumi, taarifa kutoka kampuni ya TECNO zinaeleza kuwa TECNO CAMON 16s ina kamera nne nyuma na kamera kuu ikiwa na 48MP.

 

Kamera hiyo yenye uwezo wa kuchukua picha ang’avu bila kujalisha mazingira au muda ambao picha inapigwa hata kwenye mwanga hafifu simu hiyo ina uwezo wa kupiga picha ang’avu kutokana na flashi zake nne za nyuma pamoja na lensi yenye teknolojia ya AI ambapo vyote kwa pamoja vinamsaidia mtumiaji wa simu hii kupata picha ang’avu hata kwenye mazingira yenye mwanga hafifu.

                                

 

Pamoja na kuwa na kamera kubwa yenye uwezo, pia simu hiyo imedokezewa kuwa ina memori kubwa inayofikia GB 128 ROM kwa GB 4 RAM  Ukubwa wa memori ya simu hii utamsaidia mtumiaji kuhifadhi vitu vyake bila kufuta pia kuiwezesha simu kufanya kazi kwa ufanisi zaidi bila kukwama.

 

Vilevile simu hiyo ya TECNO CAMON 16s ina Skrini kubwa ya inchi 6.6 itakayompa mtumiaji furaha na uhuru wa kutazama video, kucheza gemu pamoja na kupiga picha zinazojitosheleza na kuenea vizuri kwenye screen ambazo zitakuwa zinaleta uhalisia wa picha halisi.

 

Leave A Reply