The House of Favourite Newspapers

Tegete: Siiumbui Yanga, nafunga kwa ajili ya timu

0

STRAIKA wa zamani wa Yanga, Jerry Tegete amefunga mabao manne katika Ligi Kuu Bara akiichezea Mwadui FC sasa, hata hivyo hafungi kwa sifa bali anaisaidia timu yake iwe katika nafasi nzuri.

Tegete aliyeachwa na Yanga msimu uliopita kwa madai ya kushuka kwa kiwango, ameonyesha uwezo mzuri wa kufunga akiwa na Mwadui na kuacha maswali kuwa ilikuaje hadi akaachwa.

Straika huyo aliliambia Championi Jumamosi kuwa, makali yake ya ufungaji yasitafsiriwe vibaya kwani anachofanya ni kujituma na kufunga mabao kwa ajili ya timu yake na siyo ili aonekane yupo vizuri.

Tegete aliyeichezea timu yake mechi mbili na kufunga mabao manne, alisema: “Nacheza kwa ajili ya kuisaidia timu yangu katika harakati za kupambana kwenye ligi na si kingine kama wengine wanavyodai.

“Huwa nafurahi kila timu yangu inapofanya vizuri na namuomba Mungu atuongoze tufanikiwe kwani yeye ndiye kila kitu.”

Wakati huohuo, kocha wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ alisema Simba na Yanga zimekuwa zikiua vipaji vya wachezaji kwani ukiangalia kikosini kwake wachezaji wengi wametoka kwenye timu hizo na wanafanya vizuri.

Leave A Reply