The House of Favourite Newspapers

TEMEKE: WANAFUNZI WAWILI WAFARIKI KWA KUANGUKIWA NA UKUTA

WANAFUNZI wawili wa Shule za Msingi Kijichi na Shule ya Msingi Bwawani zilizopo Mtoni Kijichi wilayani Temeke jijini Dar es Salaam wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta wa jengo la moja ya madarasa ya Shule ya Msingi Bwawani leo Alhamisi, Desemba 6, 2018 asubuhi.

Ajali hiyo ya kuanguka kwa ukuta imetokea katika Shule ya Msingi ya Kijichi ambapo pia wanafunzi watatu wa Shule hizo wamejeruhiwa kulazwa katika Hospitali ya Temeke kwa ajili ya matibabu.

Waliokufa ni Sabra Stambuli (10) wa shule ya Bwawani na Nasri Mjenge (8) wa Shule ya Kijichi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Andrew Masatya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo. Endelea kufuatilia taarifa zetu kwa habari zaidi.

 

BREAKING: MBOWE Afikishwa Mahakamani, Arudishwa GEREZANI!

Comments are closed.