TESSY KAWAZIBA MIDOMO WANAOSEMA ANADANGA

Tessy Abdul

BE inspired! Mzazi mwenza wa staa wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka ‘Dogo Aslay’ aitwaye Tessy Abdul almaarufu ‘Tessy Chocolate’ amewaziba midomo wanaomsema kuwa anadanga baada ya kufungua bonge moja la saluni ya kike aliyoipa jina la Tessies Touch iliyopo Sinza- Kumekucha jijini Dar.  Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Tessy alisema anamshukuru Mungu kwa hatua aliyoifikia kwani siku nyingi alikuwa akiwaza kumiliki biashara yake mwenyewe hivyo anawaomba Watanzania wamuunge mkono.

“Unajua hii ni kazi ambayo ninaipenda kwa muda mrefu sana. Nimeamua kufungua saluni ili kuwaziba midomo wale wote wanaodhani ninadanga ndiyo nipendeze au nipate mkwanja,” alisema Tessy ambaye mtoto wake wa kiume na Aslay anaitwa Moza.

Stori: Memorise Richard, Dar


Loading...

Toa comment