The House of Favourite Newspapers

TET Yawasilisha Mtaala Mpya Katika Mkutano wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Msingi

0
Mkurugenzi Idara ya Ubunifu na  Ukuzaji Mitaala kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Godson Lema amewasilisha anzia mwaka Januari, 2024.
Dkt. Lema amefanya wasilisho hilo leo Novemba 9, 2023 katika Mkutano Mkuu wa tano wa umoja wa walimu wakuu wa shule za msingi Tanzania bara (TAPSHA) Jijini Dodoma.
Katika wasilisho hilo Dkt. Lema ameeleza mtaala huu unamwandaa mwanafunzi mapema juu ya kujiajiri au kuajiriwa kwani umejumuisha elimu ya amali (fani) na elimu ya jumla kwa pamoja.
Ameendelea kusema kuwa, wasilisho hili kwa Wakuu wa shule za msingi limekuja wakati muhafaka ambapo tayari Serikali imetangaza kuanza kutekelezwa kwa mtaala huu ifikapo mwaka 2024.
Aidha, Dkt. Lema amewataka Walimu Wakuu wote nchini kuupokea mtaala huo na kuwa tayari kuutekeleza pindi muda utapofika ili kuwasaidia kupunguza changamoto ya ajira kwa wanafunzi nchini.
Sambamba na hilo, Dkt. Lema amewatoa hofu Wakuu wa shule juu ya utekelezaji wa mtaala huo, huku akisisitiza Serikali imejipanga vizuri katika kuhakikisha wanafunzi wananufaika na mtaala huo ikiwemo upatikanaji wa vitabu vya kiada ambavyo viko katika hatua ya uchapaji mkubwa.
Leave A Reply