The House of Favourite Newspapers

TFF, BODI YA LIGI Mmeona Kinachotokea Kenya?

0

SHU kubwa ambayo inagonga vichwa vya wapenda michezo wote Afrika Mashariki na Kati, ni juu ya Shirikishio la Soka Kenya (FKF) kusitisha ligi yao na kuwapa ubingwa Klabu ya Gor Mahia.Kenya wameweka historia ya kuwa taifa la kwanza Afrika Mashariki na Kati, kusitisha ligi yake na ubingwa kuipa timu ambayo inaongoza ligi.

 

Uamuzi huo umeifanya Kenya ishike nafasi ya tatu kutoka Afrika ambao wamechukua uamuzi huo, wengine ni Angola na Guinea.

 

Rais wa FKF, Nick Mwendwa amejikuta akiingia katika mgogoro mzito na Bodi ya Ligi ya Kenya kutokana na maamuzi hayo, ambapo viongozi wa Bodi ya Ligi wanadai kuwa hawawezi kukubali uamuzi huo kwa kuwa hawakushirikishwa.

 

Kinachotokea Kenya kinaweza kikaikumba Tanzania, kama tu Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Almas Kasongo hawatakuwa pamoja katika kufanya maamuzi ya nini kifanyike kama hali ya Corona itaendelea kuwa hivi.

 

Mijadala imekuwa mingi kwa wadau wa michezo Tanzania ambao kila mmoja anasema lake juu ya mustakabali wa ligi yetu, wapo wanaosema ligi ifutwe na ubingwa kupewa Simba, huku wengine wakidai hakuna kanuni ya TFF, inayoruhusu Simba kupewa ubingwa.

 

Rai yangu kwa TFF na Bodi ya Ligi ni kwamba jaribuni kutumia busara katika kufanya maamuzi, ikibidi wahusisheni na viongozi wa klabu zote, hadi Ligi Daraja la Pili katika kujadili nini kifanyike kama hali itabaki kuwa hivi.

 

Simba kupewa ubingwa sawa, ligi kufutwa nayo ni sawa, lakini haiwezi kuwa sawa, kama baadhi ya viongozi watasema hiyo siyo sawa, Karia na Kasongo ndiyo ambao mmeshikilia makali, huku klabu zikiwa zimeshika mpini.basi fanyeni kwa busara, kwa maridhiano ya pande zote.

Leave A Reply