The House of Favourite Newspapers

TFF Yaingia Makubaliano Na Azam Tv Miaka 10 -Video

0
Rais wa TFF, Wallace Karia.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi na Azam TV Limited kwa pamoja leo Mei 25, 2021 wameingia makubaliano ya kuonesha matangazo ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa muda wa miaka 10.

Makubaliano hayo ambayo wameingia nao yana thamani ya Shilingi bilioni 225.6.

Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari pamoja na viongozi waalikwa waliokuwa katika hafla hiyo ya kutia saini mkataba wa Haki za Television, (Tv Rights) katika Hotel ya Hyat iliyo Posta, Rais wa TFF, Wallace Karia amesema:”Nachukua fursa hii kuwapongeza Azam Media Limetide chini ya Mkurugenzi wao Tido Muhando kwa kufanikiwa kushinda tena zabuni hii hivyo kufanya kazi na TFF pamoja na Bodi ya Ligi Tanzania, chombo ambacho kimepewa mamlaka ya kuendesha ligi hii,”.

Bonasi kwa vilabu vya Ligi Kuu kwa kila nafasi katika msimamo wa ligi; Bingwa Sh500 Mil, Nafasi ya pili Sh250 Mil, Nafasi ya tatu Sh225 Mil, Nafasi ya nne Sh200 Mil, Nafasi ya tano Sh65 Mil, Nafasi ya sita Sh60 Mil, Nafasi ya saba Sh55 Mil, Nafasi ya nane Sh50 Mil

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi wa baadhi ya klabu za Ligi kuu wamesema udhamini wa Azam unakwenda kunogesha upinzani kwenye Ligi msimu ujao.

Wamesema sasa klabu ambazo zilikuwa na changamoto ya kipato zina uhakika wa pesa za kuendesha klabu, kulipa mishahara na hata kusajili kutokana na udhamini huo.

Ofisa Mtendaji mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alisema, sasa kwenye Ligi hakutakuwa na timu ndogo wala kubwa.

“Hata zile klabu ndogo sasa zitamudu kufanya usajili wa ushindani, ila kilichonifurahisha zaidi ni bonusi ambayo klabu zitakuwa zikipewa kila msimu,” amesema na kuongeza.

“Siangalii tu kwa Simba, lakini kwa klabu nyingine pia, vilevile pesa ya udhamini iliyotolewa ukipiga hesabu ya haraka haraka, kila klabu itakuwa ikipata Sh 40 Milioni kwa mwezi ni pesa ambayo kwa kiasi fulani itasaidia,” amesema.


Leave A Reply