The House of Favourite Newspapers

Bunge la Uganda Lapata Spika Mpya

0

JACOB Oulanyah, Mbunge wa Kaunti ya Omoro Kaskazini mwa Uganda, ameteuliwa kuwa Spika wa Bunge la 11. Alishinda uchaguzi kwa jumla ya kura 310.

 

Bw. Oulanyah anachukua nafasi ya Rebecca Kadaga, aliyekuwa Spika wa kwanza mwanamke nchini humo, ambaye alishikilia wadhifa huo kwa miaka 10. Pia alikuwa mbunge kwa zaidi ya miaka 30.

 

Kinyang’anyiro cha kutafuta Spika kilisababisha mvutano ndani ya chama tawala cha NRM, huku wakosoaji wa Kadaga wakisema ameshikilia nafasi hiyo kwa muda mrefu.

 

Wikendi iliyopita, chama hicho kilimuidhinisha Oulanyah, ambaye alikuwa naibu wa Kadaga kuwa mgombea wake katika kinyang’anyiro hicho. Kadaga pia alishiriki uchaguzi huo kwa kuzingatia uwezo wake binafsi lakini hakufanikiwa.

 

Kufuatia uchaguzi wa mwezi Januari, Uganda sasa ina bunge kubwa zaidi la wajumbe 529. Wabunge pia watamchagua naibu wa Spika katika kikao chao cha kwanza ambacho kilifanyika katika Uwanja wa Uhuru wa Kololo, ili kudhibiti maambukizi ya corona.

Leave A Reply