The House of Favourite Newspapers

TFF YASHUSHA RUNGU YANGA, YAWAFUNGIA VIGOGO WAWILI – VIDEO

KAMATI ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa Mwenyekiti wake Hamid Mbwezeleni imewafungia wanachama wawili ambao ni Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Bakili Makele na Mwenyekiti wa Matawi wa klabu hiyo, Boazi Kupilika kutojihusisha na masuala ya michezo kutokana na utovu wa nidhamu.

 

Wanachama hao wamefungiwa kifungo cha miaka mitatu kila mmoja kutojihusisha na masuala ya michezo huku wakitakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 2 kila mmoja kutokana na kuhamasisha wanachama kutofanya uchaguzi.

 

Zembweleni amesema kuwa, hatua hiyo imeafikiwa baada ya wanachama hao kupinga maamuzi ya Serikali na maelekezo ya TFF juu ya uchaguzi wa klabu hiyo.

 

“Tumewafungia Bakili Makele na Boaz Kupilika kwa muda wa miaka mitatu kutojihusisha na masuala ya michezo ndani na nje ya nchi na kutoa faini ya shilingi milioni mbili kutokana na kusigana katiba ya Yanga pamoja na TFF.

 

“Tumewafungia kwa makosa mawili ya kupinga maamuzi na maelekezo ya TFF ya uchaguzi wa klabu ya Yanga, pia kuongea maneno yenye mgongano na maslahi ya TFF jambo ambalo si sahihi, wanatakiwa wakaisome katiba yao wenyewe ya Yanga waone inaeleza nini,” alisema Zembweleni.

Comments are closed.