The House of Favourite Newspapers

TGNP WAJA NA KAMPENI YA ‘LINDA MTOTO’

Ofisa wa Program Idara ya Maarifa, Tafiti na Uchambuzi wa Mtandao wa Kijinsia nchini (TGNP), Bi. Clara Gadson akizungumza kwenye mkutano huo.

MTANDAO wa kijinsia nchini (TGNP) umeadhimira kuandaa kampeni ya ‘Linda Mtoto’ katika mazingira hatarishi ikiwa ni pamoja na ngono,  kama vile watoto kubakwa na kulawitiwa, mambo  yanayowaharibia siku zao za baadaye kutokana na ukatili huo. 

Mmoja wa wanakamati wa kampeni ya ‘Linda Mtoto’ iitwayo 155, Agnes Lukanga,  amesema kuwa wameandaa kampeni hiyo ili kila mmoja katika kikundi aongee na watu watano na endapo patabainika kuwepo ukatili wowote kwa mtoto au kumkuta katika mazingira hatarishi, aweze kumlinda.

Mdau akichangia mada katika mkutano huo.
Baadhi ya wadau  kwenye mkutano huo wakisiliziza kwa umakini.

“Tumeona tuanze na kampeni hii kubwa na siku maalumu itakuwa ni tarehe 27 Februari mwaka huu, ambapo tutaifanya kwa nguvu zote na kila mwanakikundi anatakiwa awe na moyo wa kusaidia kwa dhati kwa sababu leo kitendo cha ukatili kafanyiwa mtoto wa jirani yako, kesho anafanyiwa mtoto wako,  ina maana baada ya miaka ishirini ijayo tutakuwa na kizazi ambacho hakitaelezeka endapo mtoto wa kike atabakwa na mtoto wa kiume atalawitiwa.

“Tumekuwa tukipiga vita mimba za utotoni na sasa ni wajibu wetu kupiga vita pia dhidi ya watoto na pia kwa wale wazazi ambao watoto wao wanafanyiwa vitendo hivyo na wanafamilia halafu wanaficha kwa kuepuka aibu, waseme wazi ili kuona janga hili linatokomezwa kabisa,”alisema Agnes.

Matukio katika picha:

Stori:Neema Adrian

Comments are closed.