The House of Favourite Newspapers

TGNP Yatoa Semina ya Kujadili Bajeti ya Mrengo wa Kijinsia

0
Wadau wakiwa makini kwenye semina hiyo. 

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umefanya semina kujadili ufahamu wa wadau kutoka kata mbalimbali jijini Dar, kuhusu bajeti yenye mrengo wa kijinsia ili kuwasaidia kujua namna inavyoandaliwa.

Akizungumza wakati wa semina za jinsia na maendeleo ya jamii (GDSS) ambazo huwa zinafanyika kila Jumatano, mwezeshaji wa semina na maendeleo, Thabitha Elias alisema, kunakuwa na uchambuzi wa kijinsia ambao unaweka bayana mpango wa kijinsia.

“Ni lazima kuwe na mnyambuliko wa kijinsia ambao unaanzia chini kwa kukusanya data ili kuweza kujua ni namna gani jamii itawezeshwa katika mambo mbalimbali ikiwemo maji, elimu, miundombinu, afya na mambo mengine kwa jinsia zote,” alisema.

Mmoja wa wawezeshaji akitoa somo.

Naye Ofisa Program wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Jackson Malangalila alisema, walikuwa wakiwajengea washiriki uwezo ili waweze kufanya uchambuzi wenye mrengo wa kijinsia.

“Kila mwanajamii anatakiwa awe anafika ofisi za kijiji au Serikali za mtaa ili kushiriki katika mchakato unavyoandaliwa kwa ajili ya kupanga bajeti ili kujua kama inakidhi mahitaji ya walengwa,” alisema.

Kwa upande wake, mmoja wa washiriki, Fransinca Sylivester alisema, alikuwa hana uelewa wa muhimu kwa kila mtu kuchangia bajeti, lakini baada ya semina hiyo alipata uelewa ambao ataupeleka kwa wengine.

Stori picha na mwandishi wetu

Leave A Reply