The House of Favourite Newspapers

The angel of Darkness 24

1

Magaidi walioshambulia katika kituo kikubwa cha biashara cha Kikuyu Mall jijini Nairobi, Kenya wanasababisha vifo vya watu wengi, wakiwemo Joseph Ndaki, Meneja wa Benki Kuu ya Tanzania, Tawi la Dar es Salaam na mkewe, Asia Mustafa.

Baada ya Watanzania hao kufa, wanawaacha yatima watoto wao mapacha, Arianna na Brianna ambao kila mmoja anapitia maisha ya tofauti kabisa na mwenzake.

Arianna anaokotwa na vikosi vya uokoaji na kurejeshwa Tanzania wakati Brianna anaokotwa na mwanamke mwendawazimu, Mashango na kwenda kuishi naye kwenye mtaa wa watu maskini jijini Nairobi uitwao Mathare.

Kila mmoja anapitia mitihani ya aina yake maishani mwake. Brianna, yeye analelewa na familia ya kimaskini ya mzee Njoroge, Mathare jijini Nairobi baada ya Mashango kufariki dunia kwa kugongwa na gari.

Anapohitimu darasa la saba, anakosa mtu wa kumlipia masomo ya sekondari na kusababisha arudie kwenye biashara aliyokuwa anafanya na marehemu Mashango ya kuuza mbogamboga na matunda.

Kwa upande wa Arianna, yeye anaharibikiwa kabisa kimaisha na kuwa mtumiaji mkubwa wa dawa za kulevya, anauza kinyemela nyumba aliyoachiwa na wazazi wake na kutorokea Arusha akiwa na Diego, kijana aliyekuwa akifanya biashara ya madawa ya kulevya.

Akiwa Arusha, anapata bahati ya kipekee ya kukutana na mfanyabiashara mkubwa wa madini ya Tanzanite, Msuya ambaye anampenda kwa dhati na kutaka kuyabadilisha maisha yake. Wanakubaliana wamdanganye mfanyabiashara huyo kwamba Arianna na Diego walikuwa ndugu wa damu wakati ukweli ni kwamba wawili hao ni wapenzi.

Uongo wao unafanikiwa na hatimaye wawili hao wanahamia kwenye jumba la kifahari la Msuya. Mwanaume huyo anamwambia Arianna wakapime afya zao ili mipango ya ndoa ifuatie, jambo linaloonesha kumshtua mno msichana huyo.
Je, nini kitafuatia? SONGA NAYO…

Nyendo zake na aina ya maisha aliyoishi tangu alipovunja ungo, vilimfanya Arianna awe na wasiwasi mkubwa juu ya afya yake kwani kipindi alipokuwa akianza kutumia madawa ya kulevya, alikuwa akilewa na ‘kuzimika’, hali iliyokuwa inasababisha wanaume wengi kumuingilia kimwili, tena bila tahadhari yoyote. Pia hakumuamini kabisa Diego kutokana na nyendo zake.

“Vipi mbona kama umezama kwenye mawazo? Nimekuudhi?” alihoji Msuya baada ya kumuona Arianna amebadilika, kauli hiyo ndiyo iliyomzindua msichana huyo mrembo kutoka kwenye dimbwi la mawazo, akashtuka na kukaa vizuri.

“Hapana hujaniudhi chochote, nimewakumbuka wazazi wangu, natamani wangekuwepo kushuhudia jinsi binti yao ninavyoenda kuolewa,” Arianna alimdanganya Msuya na kubadilisha kabisa mada. Hakuna jambo alilokuwa analiogopa kwa wakati huo kama kwenda kupima afya.

Waliendelea na mazungumzo ya kawaida mpaka walipokuja kuitwa na mfanyakazi wa ndani akiwataarifu kwamba chakula cha jioni kilikuwa tayari. Wakatoka na kwenda sebuleni ambapo waliungana na Diego mezani kupata chakula kizuri ambacho si Arianna wala Diego aliyewahi kukila.

Baada ya kumaliza kupata chakula cha usiku, walihamia upande wa pili wa sebule hiyo ya kisasa na kuanza kutazama runinga, huku wakiendelea na mazungumzo ya hapa na pale. Saa zikawa zinayoyoma na hatimaye ukawadia muda wa kila mmoja kwenda kulala.

Kwa kuwa kila mmoja alishapewa chumba chake, waliagana na Diego akaenda chumbani kwake wakati Msuya akimsindikiza Arianna kwenda chumbani kwake. Kila alipokuwa anakumbuka suala aliloambiwa na mwanaume huyo jioni ya siku hiyo kuhusu kwenda kupima afya zao kabla ya kuanza michakato ya ndoa, Arianna alijikuta akikosa raha kabisa.

“Hapa dawa yake ni moja, vinginevyo naweza kukosa vyote,” aliwaza Arianna wakati Msuya akimsindikiza kuelekea chumbani kwake.

“Haya ulale salama mpenzi wangu,” alisema Msuya na kumbusu Arianna kwenye paji la uso, wakiwa ndani ya chumba maalum ambacho kiliandaliwa kwa ajili ya Arianna, Msuya akataka kutoka kuelekea kwenye chumba chake ambacho kilikuwa ghorofani lakini Arianna hakumruhusu kirahisi.

“Kwani unawahi nini jamani mume wangu mtarajiwa,” alisema Arianna huku naye akimbusu mwanaume huyo kwenye shavu lake.

“Nataka nikuache upumzike, najua umechoka mpenzi wangu.”
“Usiondoke bwana, nataka unisubiri mpaka nikaoge, unibembeleze nilale ndiyo na wewe uondoke,” alisema Arianna kwa sauti ya kudeka, Msuya akawa anachekacheka mwenyewe kwa furaha. Mapenzi aliyokuwa nayo kwa binti huyo mrembo yalimfanya asiwe na ujanja wa kukataa chochote alichoambiwa, akatii alichoambiwa na Arianna.

“Hivi ukinioa utakuwa unanipenda kweli? Maana wanaume wengi wanakuwa waongo sana, akishapata anachokitaka basi anaanza kukushusha thamani.”

“Arianna niamini mpenzi wangu, nakupenda kuliko kitu chochote chini ya jua, nipo tayari kufanya chochote ilimradi nikuone ukifurahi,” alisema Msuya kwa upole, kauli iliyomfurahisha mno Arianna, akamkumbatia mahaba na kumbusu tena shavuni.
“Naomba unisubiri nikaoge mpenzi wangu.”

“Usijali, sitaondoka mpaka nihakikishe umelala kabisa kama mwenyewe unavyotaka,” alisema Msuya, Arianna akafungua begi lake dogo na kutoa khanga, akavua blauzi aliyokuwa amevaa na kubaki na sidiria, akajifunga khanga na kumalizia kuvua sketi aliyokuwa ameivaa.

Msuya alijifanya yupo mbali kimawazo, hakutaka hata kumtazama Arianna, msichana huyo akatembea kimadaha kueleka kwenye bafu lililokuwa ndani kwa ndani huku moyoni mwake akijiapiza kuwa ni lazima usiku huo afanye mapenzi na mfanyabiashara huyo ili kukwepa kipengele cha wawili hao kwenda kupima afya zao.

Dakika kadhaa baadaye, Arianna alitoka bafuni akiwa amejitanda upande wa khanga lakini tofauti na mwanzo, safari hii ndani hakuwa na kitu kingine chochote ndani. Katika hali ambayo hata mwenyewe alishindwa kuelewa imetokeaje, Msuya alijikuta akimdolea macho msichana huyo mrembo, akabaki amepigwa na butwaa akiwa ni kama haamini alichokuwa anakiona.

“You are soo beautiful Arianna!” (Wewe ni mrembo sana Arianna) alisema Msuya kwa sauti ya kukwaruza huku akimeza mate kama fisi aliyeona mfupa.

Ukiachana na kasoro zake za kitabia, ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya, Arianna alikuwa msichana mrembo sana. Weupe wake wa asili na umbo lenye mvuto wa kimahaba, achilia mbali kifua chake kichanga kilichokuwa kimechomoza kwa mbele, zilikuwa miongoni mwa sifa ambazo hakuna mwanaume aliyekamilika angeweza kujizuia kumpenda.

“Im yours Msuya, take me!” (Mimi ni wako Msuya, nichukue) alisema Arianna kwa sauti iliyotokea puani, Msuya akainuka pale alipokuwa amekaa na kumsogelea Arianna, taratibu akamkumbatia na wawili hao wakagusanisha ndimi zao, wakawa wanafanya kama njiwa anavyoyalisha makinda yake.

Kwa makusudi kabisa, Arianna aliiangusha khanga aliyokuwa amejifunga na kusababisha umbo lake zuri lionekane, Msuya akajikuta akizidi kuwa kwenye wakati mgumu. Japokuwa chumba hicho kilikuwa na kiyoyozi, kijasho chembamba kilikuwa kikimtoka Msuya huku mapigo ya moyo wake yakienda mbio kuliko kawaida. Moyoni Arianna akawa anachekelea kwani hatimaye Msuya alikuwa amenasa kwenye mtego wake.

Taratibu akaanza kumfungua vifungo vya shati lake, akahamia kwenye mkanda wa suruali yake na kuendelea na utundu wake, muda mfupi baadaye, wote wawili walikuwa kama walivyotoka kwenye matumbo ya mama zao, Msuya akambeba Arianna juujuu na kumbwaga juu ya kitanda kikubwa kilichokuwa ndani ya chumba hicho.

Hakuna kilichosikika ndani ya chumba hicho zaidi ya miguno ya hapa na pale wakati wawili hao wakijiandaa kuingia kwenye mechi ya kirafiki, isiyo na jezi wala refa. Kwa mara ya kwanza wawili hao wakajikuta wakielea kwenye ulimwengu mwingine tofauti kabisa.

Saa kumi na moja alfajiri iligonga wawili hao wakiwa wamelala fofofo ndani ya chumba cha Arianna, Msuya ndiye aliyekuwa wa kwanza kushtuka usingizini na kujikuta amelala na Arianna, wote wakiwa kama walivyoletwa duniani.

Harakaharaka akaamka na kuvaa nguo zake, akafungua mlango taratibu na kunyata kuelekea chumbani kwake kwani hakutaka mtu yeyote ajue kilichotokea usiku huo. Akapitiliza mpaka bafuni ambapo alijimwagia maji na kurudi kitandani kwake, akaanza kutafakari kilichotokea usiku huo.

Japokuwa ndani ya nafsi yake alikuwa akijilaumu kwa kukutana na Arianna bila hata kuchukua tahadhari yoyote, upande mwingine alijipongeza kwani alichokuwa amekihisi tangu siku ya kwanza alipoonana na msichana huyo hakuwa amekosea kumchagua.

kajiapiza kuwa atafanya kila kinachowezekana ili kuhalalisha uhusiano wao. Alikuwa ni kama amelamba asali na sasa alikuwa tayari kuchonga mzinga, hakukumbuka tena suala la kwenda kupima afya zao.

Je, nini kitafuatia? Usikose Jumatatu kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda.

1 Comment
  1. ahady kidehele says

    haya kaz kwako msuya

Leave A Reply