The House of Favourite Newspapers

Tiboroha Azindua Kampeni za Uenyekiti Yanga

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha (katikati),  akizindua kampeni zake za kuwania nafasi ya Mwenyekiti katika klabu ya Yanga.

ALIYEWAHI kuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Jonas Tiboroha,  hatimaye leo amezindua rasmi kampeni zake za kuwania nafasi ya mwenyekiti katika klabu hiyo.

 

Katika uzinduzi huo uliyofanyikia makao makuu ya klabu hiyo amewatambulisha baadhi ya wajumbe wanane atakaoambatana nao, ambao ni Ally Msigwa, Christopher Kashililika, Dominic Francis na Salim Rupia.

 

Wengine ni Arfat Hadji, Said Barala na Peter Simon ambao wote ni wanagombea katika nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo.


Tiboroha ameanika vipaumbele vyake kuwa akipewa ridhaa ataanza na kujenga na kuimarisha taasisi hiyo,  pili atafanya juhudi za haraka kuirudisha klabu kwa wanachama na mashabiki wake.

 

Pia amesema  atafanya kazi ya kuimarisha matawi, atajenga mara moja misingi ya uwekezaji na biashara, kuimarisha na kujenga mifumo ya klabu na kushirikisha wadau wote.

HABARI/PICHA ; MUSA MATEJA | GPL

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

KARIBU ujiunge na familia ya marafiki wa Global TV Online – Club sasa, uwe wa kwanza kupata video zote za Global TV, video za hamasa kutoka kwa Eric Shigongo, breaking news za matukio yote duniani, michezo na dondoo za afya. Utapata nafasi ya kuingia bure na kutazama shoo, matamasha, semina na burudani zinazoandaliwa na Global TV mikoa yote Tanzania.
Pia, ukiwa na tatizo la kifamilia mfano misiba, kuuguliwa na majanga, marafiki zako wa Global TV Club tutakusaidia.
 
Pia, tutakuunganisha na mtandao wa marafiki zetu waliyofanikiwa ndani na nje ya Tanzania, ili upate mafunzo maalum ya kujikwamua kutoka katika hali duni ya maisha.

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.