The House of Favourite Newspapers

TID Mnyama Kuachia Kombora la Albam

0

LEGENDARI wa muziki wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed ‘TID’ ametangaza kuachia albam yake mpya na ya sita amabyo ameipa jina la #NiYeyeAlbum ambayo itatoka siku za hivi karibuni.

 

Akizungumza na moja ya media hapa Bongo, Mnyama amesema; “Nakuja na albam na nimesema hii albam inaitwa #Niyeye na nitashirikisha wakali wangu wote ambao naamini kwamba watatengeneza album nzuri.

 

“Albam ni feelings siwezi nikakurupuka tu nikasema natengeneza albam, nimeanza kurekodi kitambo na bado naendelea kurekodi.

“Kwahiyo mwaka huu nakuja na albam yangu ya #Niyeye ambayo wimbo wa kwanza ndio huo #Macho na kuna kazi nyingine zitatoka soon hivyo wakae mkao wa kula, ni wakati wa watu kuusikia muziki wetu,” amesema TID.

Leave A Reply