The House of Favourite Newspapers

TIFFAH WA ZARI AITIKISA DUNIA

DAR ES SALAAM: Ametisha sana! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mtoto wa mjasiriamali mashuhuri Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Tiffah kuwa na wafausi wengi zaidi kuliko watoto wengi wa mastaa wakubwa duniani.

Tiffah ambaye Zari amezaa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, aliibua gumzo la aina yake juzi, mara baada ya baba yake kumposti katika ukurasa wake wa Instagram na kumtambulisha kama mtoto pekee wa kike mwenye wafauasi wengi duniani.

“Most followed female kid in the World,” aliandika Diamond ujumbe huo uliosindikiza kipande cha video kilichomuonesha Tiffah akiwa amekaa akichezea rundo la viatu vyake vilivyokuwa vinamzunguka.

WAUASI WA TIFFAH INSTA

Tiffah mwenye umri wa miaka 2 na nusu, ana wafuasi Milioni 1.8 katika ukurasa wake wa Instagram ambao wazazi wake walimfungulia tangu alipozaliwa.

MITANDAONI KWACHAFUKA

Mara baada ya Diamond kutupia video hiyo na kusindikiza na ujumbe wake, mtandaoni kulilipuka na kila mtu kueleza mtazamo wake juu ya kauli ya ‘Most followed female kid in the world’.

WENGINE WAMTETEA

Kuna ambao walionekana kumtetea Diamond kuwa amesema kweli kwamba hakuna mtoto yeyote wa kike wa staa duniani mwenye wafuasi wengi mtandaoni zaidi yake lakini kuna ambao waliponda kwa kusema si kweli.

HOJA ZA WALIOPONDA

Walionekana kuponda mitandaoni, walisimamia hoja yao kwa kusema kwamba kuna watoto wa mastaa maarufu Marekani ambao wanaamini wana wafausi wengi kuliko Tiffah.

MANENO MAKALI

Bila kuwa na ‘data’ za kuthibitisha, wafuasi hao walicharuka kwa kusema katika hali ya kawaida, mtoto wa Zari na Diamond hawezi kuwa na wafuasi wengi zaidi kuliko mtoto wa Jay Z na Beyonce wa Marekani.

Wengine walienda mbele zaidi kwa kusema mtoto wa Kanye West na Kim Kardashian kumpambanisha na mtoto wa Diamond na Zari ni kama ardhi na mbingu kwani watoto hao wanabebwa zaidi na umaarufu wa wazazi wao.

“Katika hali ya kawaida, Zari na Mond (Diamond) wanaweza kuwafikia Kim na Kanye? Tuache masihala jamani, huu ni ujinga kuwapambanisha Tiffah na North wa Kanye West au Tiffah na Blue Ivy wa Jay Z na Beyonce,” alichangia mdau mtandaoni.

MJADALA NCHI MBALIMBALI

Posti hiyo ilionekana kugonga nchi mbalimbali kwani uchunguzi uliofanywa na Risasi Mchanganyiko kwa kuzifuata akaunti za wachangiaji mbalimbali, ulibaini maoni hayo yamechangiwa na wachangiaji wa nchi mbalimbali.

WENGINE WATOKA

NJE YA MADA

Wengine badala ya kuchangia mjadala wa msingi wa kukubaliana na kauli ya Diamond au kuipiga, walitoka nje ya mada hiyo na kuanza kujadili ishu ya vitabu vya dini vilivyoonekana kwenye kipande cha video alichokiposti staa huyo wa Bongo Fleva.

“Jamani jamani huyu Diamond vipi? Anamuwekeaje mtoto vitabu viwili vya dini Msahafu na Biblia? Mtoto sasa afuate kitabu gani? Haoni kama atakuwa anamchanganya mtoto?” alichangia mmoja wa wafuasi wa Instagram ambaye naye alipata wapambe wa kumuunga mkono.

MTOTO WA DJ KHALEED AIBULIWA

Kundi la wafuasi lililokuwa halimuungi mkono Diamond, lilimuibua mtoto wa DJ maarufu nchini Marekani, DJ Khaled, Asahd ambaye alionekana kumzidi wafuasi Tiffah ili kumkata ngebe Diamond.

WAINGIA CHAKA KIAINA

Licha ya Asahd kuwa na wafuasi Milioni 1.9 Instagram, laki moja zaidi ya wale wa Tiffah, wafausi waliomlinganisha Tiffah na Asahd waliingia chaka kiaina kwani Diamond alimaanisha mwanaye hana mpinzani kwa watoto wa kike.

RISASI MZIGONI

Baada ya kuachana na ‘tifu’ hilo la mtandaoni, Risasi Mchanganyiko liliingia mzigoni kuchimba ‘data’ mbalimbali na kujiridhisha kwamba binti huyo kweli anaongoza kwa kuwa na wafuasi wengi hususan kwa watoto wa kike wa mastaa duniani.

Mbali na watoto wa kike wa mastaa, Tiffah ameonekana kuwakimbiza pia watoto wa kiume wa mastaa ulimwenguni ukimuondoa Asahd wa DJ Khaled.

ORODHA KAMILI

Watoto wa Kanye West;

North West (north.west_) ana miaka 5, wafausi 278,000.

Saint West (itssaintwest) mwenye umri wa miaka 2, ana wafuasi elfu hamsini na sita.

Chicago West (chicago. west_) mwenye miezi 4, ana wafuasi elfu 41 na ushee.

Watoto wa Beyonce;

Blue Ivy (blueivy.carter) mwenye miaka 6, ana wafuausi 139,000.

Mtoto wa Wiz Khalifa;

Sebastian Taylor Thomas (sebastian.taylor) mwenye umri wa miaka 5, ana wafuasi 6,477.

STORI: Erick Evarist, Risasi Mchanganyiko

 

 

Comments are closed.