The House of Favourite Newspapers

Tigo, Absa Bank na Jumo Wazindua Huduma ya Mkopo kwa Muda Mfupi

0

Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha (katikati) akizungumza kwenye uzinduzi huo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu Kitengo cha Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laizer na kushoto ni Meneja Mkazi wa Jumo Tanzania, Erick Ruyanga.

 

 

 

Leo Septemba 15, 2021 Kampuni inayoongoza katika kuhakikisha Mtanzania anaishi maisha ya Kidigitali, Tigo Tanzania Kwa kushirikiana na Absa Bank Tanzania Limited na JUMO wamezindua huduma ya mkopo wa muda mfupi ijulikanayo kama ” TIGO NIVUSHE”.

Afisa Mkuu wa Tigo Pesa Bi. Angelica Pesha akifafanua jambo kwenye uzinduzi huo.

 

 

 

Akizungumza katika uzinduzi huo Afisa Mkuu wa Tigo Pesa Bi. Angelica Pesha amesema kuwa Kuanzishwa tena kwa huduma hii ya TIGO  NIVUSHE hasa safari hii kwa kushirikiana na Benki ya Absa pamoja na JUMO inadhiirisha kuwa Tigo Pesa imeendelea kuwa kinara katika utoaji wa huduma za kifedha hapa nchini wakati huohuo ikiunga mkono jitihada za serikali kupunguza pengo katika utoaji wa huduma za kifedha hasa katika kukopesha sekta ndogondogo.

Meneja Mkazi wa Jumo Tanzania, Erick Ruyanga akielezo taasisi yake itakavyohusika katika kutoa huduma hiyo.

 

 

“Mnamo mwaka 2015 tulizindua huduma hii ya TIGO NIVUSHE   Kwa  mara ya kwanza kwa kushirikiana na JUMO ambapo tuliweza kutoa mikopo  kwa wafanyabiashara wadogowadogo na wa kati pamoja na kundi jingine la wale ambao walipata shida kupata mikopo rasmi.

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Absa Tanzania Kitengo cha Fedha akieleza jinsi benki hiyo itakavyoiwezesha Tigo fedha za kuwakopesha wateja wake. Kushoto Mkuu wa Tigo Pesa Angelica Pesha akimsikiliza.

 

 

 

Tangu kuanzishwa kwa huduma hii ya TIGO  NIVUSHE tumeweza kutoa mikopo kwa zaidi ya wateja million 2.1 wa Tigo Pesa, Ushirikiano wetu na Benki ya ABSA na JUMO utafungua njia ya kutolewa mikopo zaidi Kwa wateja Stahiki wa TIGO PESA hasa kuanzia Mwezi huu wa Septemba na hii yote ni kutokana na Kampuni ya TIGO kupitia TIGO PESA kuendelea kuwajali na kuwafungulia dunia wateja wake hasa katika utoaji wa huduma za kifedha.

Mapaparazi wakiwajibika kwenye uzinduzi huo.

 

 

Wateja waliosajiliwa kikamilifu na watumiaji wa Tigo Pesa mara kwa mara wataweza kukopa kiwango cha kuanzia Tsh. 2,000 Hadi 1,000,000 kulingana na mahitaji na ustahiki Kwa muda wa mkopo wa siku 7 – 30 , na wateja wasiostahili wanahimizwa kutumia huduma za Tigo Pesa zaidi kujiongezea uwezo wa kupata mkopo, na wanufaika wa TIGO NIVUSHE wanahimizwa kutumia huduma hiyo mara kwa mara na kulipa kwa wakati ili kuongeza kiwango cha kukopa zaidi na zaidi. Alimalizia Bi Pesha

 

 

Kumbuka ili kupata mkopo wa TIGO NIVUSHE mteja anahitaji kupiga *150*01# , chagua namba 7 huduma za kifedha halafu 4 Tigo Nivushe na ufuate maelekezo, na Kwa wale wateja waliothibitishwa kuwa wanastahiki kupata mkopo huu watapiga *150*81# na kufata maelekezo.

Leave A Reply