The House of Favourite Newspapers

TIGO FIESTA KUTIMUA VUMBI ARUSHA JUMAMOSI IJAYO

0
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Tigo, William Mpinga akiongea na wanahabari kwenye mkutano huo leo.
Mkutano ukiendelea.

Tamasha la Tigo Fiesta linatarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi ijayo katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha huku wasanii kibao wakitajwa kusajiliwa kutoa burudani kwenye tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika karibu nchi nzima.

Akizungumza na Wanahabari kwenye Makao Makuu ya ofisi ya Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Kampuni hiyo, William Mpinga alisema katika tamasha hilo wasanii pendwa zaidi ya 17 tayari wameshasajiliwa akiwemo Alikiba Christian Bella, Shilole, Saida Karoli, Mr Blue, John Makini na wengineo.

Mpinga amesema kuwa wateja watakao taka kwenda kwenye tamasha hili wataweza kununu tiketi za kiingilio kwa Tigo Pesa kupitia namba 0678888888 ambapo mteja yeye atakayenunua tiketi kwa kutumia huduma hiyo atapata pinguzo la asilimia 10.

HABARI/ PICHA: RICHARD BUKOS / GPL    

 

Leave A Reply